Jumanne, Aprili 12, 2011

Naomba ushauri nina ngozi yenye mafuta

Mambo my dear naitwa Jacline mimi ninashida na naomba unishauri jamani maana mi nina oil skin san japo sina chunusi ila nina Dermatosis papulosa nigra, ukigoogle unaweza kuiona na kutoa ushauri nifanyeje na kila nikiangalia website yako nakutana na wadada/wamama nyuso zao ziko bring bring kweli. Huwa nikipaka make up inakaa vizuri na havionekani tatizo make up yenyewe hata powder haikai muda mrefu. Naomba kama unaweza pia kuwaomba wadau wako wanishauri nitumie nini ili niweze kuwa na ngozi nzuri, mi si mweupe sana ila nina ngozi laini yenye mafuta.
I have very very very very oily skin, and my makeup comes off within a few minutes, I feel like I am just wasting my makeup. I need SOMETHING that will help it stay on!  Please I really need your advice.
Samahani nimechanganya lugha maana najua wengine wanaotembeleawebsite yako hawajui Kiswahili. Mi niko Tanzania, Dar es salaa,



 Ushauri kuhusu ngozi yenye mafuta  nilishawahi kuandika kipindi cha nyuma lakini nikaona nikuwekee tena hapa uweze kusoma kwa umakini Unaponunua kipodozi cha aina yoyote lazima uangalie na aina ya ngozi uliyonayo kwani vipodozi vyote vimeandikwa aina ya ngozi na ukishajua hilo basi nunua kipodozi kinachoendana na ngozi yako kwa mtu mwenye ngozi yenye mafuta hakikisha unasafisha uso mara kwa mara na "facial clenser" tena zingatia sana kabla ya kulala uhakikishe uso wako umeusafisha vizuri,kama umekosa bidhaa hiyo unaweza kutumia hata maji.wakati unasafisha uso hakikisha unatumia kifaa laini na pia hakikisha hausugui uso kwa nguvu,maana vinginevyo utasababisha ngozi yako kuwa ngumu.
 
Hizi ni baadhi ya makeup ambazo zinapatikana madukani na inabidi kuwa makini wakati wa kununua kulingana na aina ya ngozi,tumia vipodozi ambavyo havina mafuta kabisa ambavyo ni maalumu kwa ngozi yenye mafuta,pia unaweza kupaka maji ya matango kwenye uso wako kabla ya kupaka makeup inasaidia kwenye muonekano wa ngozi 
 
Tafuta foundation ina Titanium dioxide ambayo pia inakusaidia kujikinga na jua,,ukitaka kuwa na ngozi yenye mvuto basi hii ndio siri yako kama ngozi yako ina mafuta,jaribu kuwa makini waone wataalamu kwa msaada zaidi kuliko kuiga au kubahatisha.

Maoni 1 :

Bila jina alisema ...

My dear Adela nashukuru sana kwa ushauri wako. Jack

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom