Jumatatu, Mei 23, 2011

Lainisha ngozi ya miguu yako bila ya kutumia gharama kubwa.

Miguu ni sehemu nzuri katika mwili wako ingawa watu wengi husahau miguu yao matokeo yake ngozi inakuwa kavu au inapasuka, ni muhimu kukumbuka kulainisha miguu yako mara kwa mara kwani urembo si kwenye sura peke yake bali ni kwa mwili mzima
Osha miguu yako kwa kutumia maji na sabuni hakikisha unaisugua kwa umakini ili itakate na  kisha ikaushe vizuri na taulo
Mafuta haya ya mgando ni mazuri sana katika kulainisha ngozi ya miguu yako
Baada ya kukausha miguu yako na taulo paka mafuta ya mgando katika miguu kuzunguka nyayo,vidole, kwenye mikunjo ya vifundo vya miguu na katika maeneo makavu kumbuka kutumia mafuta mengi kiasi hakikisha unapaka kwa umakini huku ukiwa unajikanda taratibu.
Baada ya hapo vaa jozi za soksi safi za pamba, halafu nenda kitandani na ulale, ni vizuri kufanya hivi usiku baada ya kuoga na asubuhi ukiamka ngozi ya miguu yako itakuwa laini zaidi. Jaribu leo na ulainishe ngozi ya miguu yako.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom