Jumatatu, Januari 16, 2012

"Tulipendana sana na tulikuwa na malengo ya kufunga ndoa lakini nilipokwenda uzazi kurudi mwenzangu amebalika kabisa"


Mimi  ni mdada wa miaka 25 nilikuwa na  mchumba tumekuwa wapenzi kwa muda wa miaka miwili  sasa nampenda sana na malengo yetu ilikuwa ni kuja kuoana  na mungu ametujalia tumepata mtoto mmoja wa kike lakini nilipo rudi kutoka uzazi mwenzangu hakuwa na mwelekeo tena yaani kabadilika kama sio yule wa kwanza  alikataa mtoto na wala hajawahi kutoa matumizi kabisa yapata miaki miwili sasa na nilipojaribu kuchunguza nikaambiwa ana mke na nilipomtumia meseji kumwambia baba vipi kuhusu mtoto maana sioni lolote aliniambia jibu la hiyo meseji liko mbali nimejaribu kuongea na mama yake mzazi ili aweze kuongea naye na mama yake kasema ameambiwa nisubiri.

sasa dada Adela naomba ushauri  kupitia blog yako nimekuwa nikimsubiria kwa muda wa miaka 2sasa na wala sioni mwelekeo kutoka kwake wala kwa mzazi wake nifanyeje jamani yaani hakuna anayenijali.

naombe ushauri wenu wadau

Maoni 2 :

Bila jina alisema ...

Mmh kwanza mpe Pole, watu wanasema kabla hujafa hujaumbika! kwa maelezo yake, inaelekea kabisa huyo Jamaa kashachokanae, na baya zaidi wazazi wa huyo Jamaa, wako Upande wa mtoto wao wa Kiume, so utakuta hapo kila sehemu kuna ugumuwake. Ila Jibu sahihi hapo ni kwamba Jamaa hamtakitena huyo Binti, na wazee wake wako radhi kwahilo. Chakufanya ni kumlea mtoto wake, na ajaribu kumsahau huyo Jamaa. najuwa ni ngumu sana na inauma, lakini hakuna la kufanya hapo, kama kashaoa, so ako na familia nyengine na wanaishi, sio rahisi kama Jamaa atamkumbuka na kumrudia. Amlee mtoto kwa wema, na sasa kitakuwa kikubwa tena miaka miwili, ajitahidi Mungu atamsaidia.

Bila jina alisema ...

pole sana mdada ila muangalie mtoto wako achana na huyo mwanamume inaonekana ni tapeli we mtunze mtoto atamtafuta mwenyewe wanajishaua tu huwaga

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom