Friday, February 24, 2012

SIMULIZI YA KOSA LANGU SEHEMU YA NNE

 AUTHOR   ADELA DALLY KAVISHE

Baada ya kifo cha Mama Joyce  maisha ya Joyce na mdogo wake yalibadilika,waliishi katika mazingira magumu bila kujua nini hatima ya maisha yao. Joyce alitamani sana mdogo wake aende shule kuendelea na masomo lakini alikuwa hana uwezo, siku moja akiwa amekaa kibarazani katika nyumba ambayo walipenda kukaa na kuomba msaada kwa watu mbalimbali Joyce aliwaza moyoni mwake akisema
“ haya maisha tutaishi hivi hadi lini nikimuangalia mdogo wangu natamani asome lakini sina uwezo wa kumpeleka shule sijui nifanyeje” aliwaza Joyce huku akimtazama mdogo wake aliyekuwa anachezea mchanga.

 Akiwa anaendelea kuwaza alijitokeza kaka mmoja akamshtua na kumwambia “Mambo vipi mrembo” Joyce aligeuka na kuitika “Salama tu kaka” yule kaka akamsogelea karibu na kusema “mbona unaonekana una mawazo sana mrembo vipi una matatizo gani?” aliuliza yule kaka, Joyce alinyamaza kimya kidogo na kusema  “Nina matatizo mengi sana kaka yangu sijui nianzie wapi kukueleza”  yule kaka aliendelea kijisogeza karibu na Joyce kisha alikaa chini “acha hizo binti mzuri kama wewe una matatizo gani, mimi naitwa Maliki sijui mwenzangu unaitwa nani” alisema Maliki huku akimtazama Joyce.

 “Mimi naitwa Joyce na yule pale ni mdogo wangu anaitwa James” Baada ya kufahamiana Maliki  akaandelea kumuuliza “Joyce umesema una matatizo gani?” Joyce alimgeukia  na kusema “Ni historia ndefu kidogo naweza kukusimulia”  ndipo kwa umakini Joyce alimueleza Maliki kila kitu kuhusu maisha yake Maliki aliwaonea huruma sana na hivyo alimchukua Joyce na mdogo wake na kwenda kuishi nao nyumbani kwake.

 Maliki alikuwa akiishi katika nyumba kubwa ambapo alikuwa akiishi peke yake. Walianza maisha mapya ya kuishi nyumba moja na Maliki aliyekuwa akiishi nao vizuri na hatimaye aliamua  kumpeleka shule James kuendelea na masomo darasa la tatu lakini kwa Joyce ilimbidi abaki pale nyumbani na kufanya kazi za ndani na Maliki alimuahidi kumlipa mshahara kila mwisho wa mwezi Joyce alifurahi sana. Baada ya mwezi mmoja tangu Joyce na mdogo wake waanze kuishi na Maliki maisha yao yalianza kuwa mazuri  lakini baadaye mambo yakaanza kubadilika kwani Maliki alianza kumtaka kimapenzi Joyce.
 Siku moja Joyce alikuwa amepumzika sebuleni akiwa anatizama tamthilia Maliki alikuwa anatoka kazini alifika na kumsalimia kisha kusogea karibu na Joyce na kusema “Joyce samahani kuna kitu nataka nikuambie naomba unisikilize kwa umakini” Joyce aliyekuwa amejilaza kwenye kochi alinyanyuka na kukaa vizuri kisha kusema “Hakuna tatizo kaka Maliki mimi nakusikiliza” 

Maliki alishusha pumzi na kumshika mikono Joyce huku akisema “Joyce mimi nakupenda sana na moyo wangu ulikupenda tokea siku ya kwanza nilipokuona naomba uwe mpenzi wangu nakuhitaji sana Joyce” Joyce aliinama kwa aibu na kusema “Mmh kaka Maliki hapana haiwezekani mimi bado mdogo sana kujiingiza katika mapenzi na wewe ni mtu mzima mimi nakuheshimu kama kaka yangu” alisema Joyce huku akiwa anatetemeka kwa kuogopa wakati huo Joyce alikuwa na miaka 16 na Maliki alikuwa ni kijana mwenye umri kati ya miaka 30 hadi 33. Baada ya Maliki kuona Joyce amekataa aliendelea kumsisitiza lakini Joyce alikuwa na msimamo
Hakukata tamaa aliendelea kumbembeleza Joyce amkubalie ombi lake la kutaka awe mpenzi wake, Joyce aliendelea kuwa na msimamo wa kukataa huku Maliki akiendelea kumuomba na kumuahidi atamsaidia kwa kila kitu pamoja na kumsomesha mdogo wake lakini msimamo wa Joyce ulimfanya Maliki ampe muda wa kumfikiria,zilipita kama siku tatu tangia Maliki amwambie Joyce kuwa anampenda kimapenzi, siku zote Joyce alikuwa akiishi huku mawazo yakiwa yamemtawala kichwani akiliwaza suala hili la Maliki.

 Ilikuwa ni mida ya saa tatu usiku Joyce alikuwa amejipumzisha sebuleni na mdogo wake alikuwa chumbani amelala wakati huo Maliki alikuwa bado hajarudi kutoka kazini,Joyce alikuwa akiangalia tamthilia  iliyokuwa inaonyeshwa katika runinga baadaye alipitiwa na usingizi na kujikuta amelala palepale sebuleni.

Baada ya muda kupita mnamo saa sita usiku Joyce alikuwa bado amejilaza sebuleni na mlango wa sebuleni ulikuwa haujafungwa, Maliki alirudi usiku huo aliingia na kumkuta Joyce akiwa amelala kwenye kochi alisimama kwa muda pale mlangoni huku akimtazama Joyce kwa umakini na moyoni mwake akisema "mmmh huyu mtoto nampenda sana embu tizama alivyolala kama Malaika, mzuri sana huyu binti namtamani" 

Akiwa anawaza huku anasogea taratibu katika kochi alilokuwa  amelala Joyce alikuwa amevalia gauni fupi na kwa namna alivyokuwa amelala sehemu ya paja ilikuwa inaonekana basi Maliki alipofika alianza kumshika pajani Joyce huku akimpapasa taratibu Joyce alishtuka kutoka usingizini na kusema "Aaah jamani kaka Maliki umenishtua" Maliki alinyanyua mkono wake wa kulia na kumshika Joyce mikono yake miwili huku akisema "Joyce mpenzi kwa nini unanitesa hivi si unajua kwa kiasi gani mimi nakupenda nahitaji penzi lako nakuomba unikubalie naahidi sintokuumiza nakupenda sana" alisisitiza Maliki huku akimpapasa Joyce viganja vya mikono yake Joyce aliyekuwa amejiinamia kwa  aibu alisema "Kaka Maliki mimi naogopa haiwezekani mimi bado mdogo,wewe niache mimi siwezi naomba unisamehe" Maliki aliyekuwa anaonekana amelegea macho huku akimtazama Joyce alimkumbatia Joyce kwa nguvu na kusema "nikupe nini mpenzi nakupenda nikubalie ombi langu".

 Joyce huku akiwa  anatetemeka alijaribu kujivuta ili ajitoe mikononi mwa Maliki bila mafanikio akiwa anaendelea kujaribu kujitoa Maliki aliisogeza midomo yake karibu na midomo ya Joyce na kuanza kumbusu kwa umakini kabisa aliendelea kumshikilia kwa nguvu baadaye alimbeba na kumpeleka Chumbani ambapo Joyce alibaki akilalamika "Kaka Maliki mimi naogopa naomba uniache unaniumiza" Alisema Joyce ambaye ilikuwa ndiyo mara yake ya kwanza kuwa katika mapenzi.

 Maliki aliyekuwa kama amechanganyikiwa hakumsikiliza aliendelea hadi alipomaliza alichokuwa anakitaka kwa Joyce kisha akaanza kumbembeleza Joyce aliyekuwa akilia kwa maumivu makali "Pole mpenzi usijali mimi nakupenda Joyce usilie nyamaza mpenzi" Joyce aliendelea kulia baadaye aliondoka huku akichechemea kwa maumivu, alienda kuoga na kurudi chumbani kwake kulala huku moyoni akiwa anawaza "siamini kama Kaka Maliki amenifanyia hivi,sijui nitoroke na mdogo wangu, mimi siwezi kuishi haya maisha, na je kama nitatoroka nitaenda wapi? Na sina mtu wa kunisaidia" aliwaza Joyce huku akiwa analia kwa uchungu.....nini kitaendelea je Joyce atatoroka au atabaki usikose sehemu ya 5.......

7 comments:

lulu ibrahim said...

hahahahhahah dahhhhhhhhh naona kama inachelewa sehemu ya sita jinsi ilivyo inasisimua na tamu

Anonymous said...

hongera Adela mtiririko mzuri sana uko juu kipenzi story inaeleweka

Anonymous said...

jamani hii simulizi imenigusa sana natamani kupata vipengele vyote kazi nzuri Adela

Anonymous said...

pamoja sana naifuatilia sana hii simulizi wangu mie Jack wa kimara nasubiri kitabu tu kitoke

Anonymous said...

asiyekubali utunzi unaweza rafiki yaani u good my dear hii inasikitisha sana

Adela Dally Kavishe said...

Asanteni sana wadau kwa kuwa pamoja nami pia ukitaka kusoma kuanzia simulizi ya kwanza ingia kwenye simulizi ya kosa langu utazipata zote ili uelewe wapi imeanzia na nini kinaendelea tuko pamoja sana

david said...

sista story imetuliya ile mbaya mbona hiyo part ya 6 imechelewa hivyo mungu azidi kukubariki.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...