Jumatano, Aprili 11, 2012

Matumizi ya asali na ukwaju katika kuondoa chunusi

Ukitaka kuondoa chunusi usoni na kusafisha uso usiwe na madoa ni vyema ukatumia njia asili kufanya hivyo tumia asali na ukwaju kupata matokeo mazuri bila madhara

Ukwaju na asali hupatikana kwa urahisi sokoni

Ipende ngozi yako wakati wote kama utaona inakuchukua muda mrefu kutengeneza mchanganyiko wa asali na ukwaju basi ni vyema vipodozi unavyonunua kama sabuni ama losheni hakikisha vimetengenezwa kwa mchanganyiko wa asali na ukwaju

Tafuta ukwaju loweka katika maji ukishalainika changanya na asali, paka usoni. muda mzuri wa kufanya hivi ni usiku  ambapo unapaka na kukaa takribani kama nusu saa kisha safisha uso wako vizuri fanya hivyo mara kwa mara kwani ni dawa nzuri sana na utaona ngozi yako inabadilika kwa kipindi kifupi.

Maoni 11 :

Bila jina alisema ...

Asante Adela kwa hili urembo wa asili ni mzuri zaidi

Bila jina alisema ...

asante dada kwa msaada wa kuwa na ngozi nzuri,naomba msaada wa vipimo nichanganye asali kwa ukwaju kiasi gani?

Unknown alisema ...

Ahsante dada kwa somo lako zuri sasa huo mchanganyiko utapaka ndani ya siku ngapi? pia naomba msaada wa vipimo nichanganye asali kwa ukwaju kiasi gani?

Unknown alisema ...

Ahsante kwa urembo wa asili usiobabua ngozi yako.

Bila jina alisema ...

Asante dada kwa ushauri wako, nitakupa matokeo

Unknown alisema ...

Dada Adela asante sana kwa ushauri wako nimejaribu kufanya ndani ya wiki 2 imenisaidia sana sina madoa wala chunusi.ubarikiwe

Unknown alisema ...

Dada Adela asante sana kwa ushauri wako imenisaidia sana na nimepaka kwa muda wa wiki 2 ngozi yangu imekua imara sina chunusi wala madoa asante na ubarikiwe.

Unknown alisema ...

Asante dada Adela kwa ushauli wako mzuri

Dinah Weddy alisema ...

Asante dada

Dinah Weddy alisema ...

Asante dada Adela

Bila jina alisema ...

Asante Adela nimepata maarifa ya urembo wa kutengeneza uso kwa asili bila madhara. Ubarikiwe.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom