Jumatatu, Mei 27, 2013

"MIMI NI MWANAUME NIMEPIMA UGONJWA WA UKIMWI NA KUJIGUNDUA KUWA NIMEATHIRIKA LAKINI NAOGOPA KUMWAMBIA MKE WANGU NAOMBENI USHAURI"

Dada Adela samahani naomba unisaidie kuomba ushauri kwa wadau wa blog yako. Mimi ni mwanaume nina umri wa miaka 38 nina mke na watoto wawili, Naipenda sana familia yangu lakini tatizo limejitokeza baada ya mimi kuwa na safiri mara kwa mara katika biashara zangu na kujikuta nikiwa mbali na familia yangu kwa muda mrefu.Wakati mwingine zaidi hata ya miezi mitano nilijikuta naanzisha mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mmoja ambaye nilikuwa nikishiri naye tendo la ndoa bila ya kinga na pia  nikirudi nyumbani nashiriki tendo na mke wangu.

  Hivi majuzi nimepima ukimwi na kujigundua kuwa nimeathirika, akili yangu imekuwa kama mtu aliyechanganyikiwa, nina  mawazo sana na pia najuta kwa yote niliyoyafanya,  nashindwa nitamuelezaje mke wangu. Kwani hapa nilipo sijui kama na yeye atakuwa ameathirika au la na pia naogopa kumpoteza mke wangu naombeni mnisaidie kwa ushauri jamani kwani sijielewi hapa nilipo.

Maoni 3 :

Bila jina alisema ...

pole sana japo kwa sasa sio wakati wa kuku-judge wewe huu sio wakati wakumtafuta mchawi ni wakati wa kumtibu mgonjwa ambaye ni wewe unayeomba ushauri japo ulifanya kosa posikutumia kinga na huku wajua wazi ukimwi upo huwezi pima ukimwi kwa macho anyway so chakufanya maji yamesha mwagika kaa chini umwombe Mungu sana akupe roho ya ujasiri uondoe hofu kwani najua unavyojifeeli na kujuta sana but now its too late chakufanya mpele mke wako hospitali usimwambie wewe umeshapima bali mwambie tu twede tukapime afya zetu tujue hali zetu so akikubali mtaeenda mpime tena upya na majibu muyapokee kama hapata maamb ukizo ni vizuri na hata kama amepata muushi kwa matumaini kwani ku7pata ukimwi sio mwisho wa maisha japo unatakiwa uwishi kwakufuata masharti utaishi maisha marefu nahuku watoto wanaendelea kukuwa usijipe hofu sana maana kinga zitashuka utaanza kuumwa haraka jikubali tu badilisha tabia na wakati wakujamiana unatumia kinga na kama unakunywa pombe uache na kutembea hovyo uwache pia na ule vizuri na mazoezi kidogo utaishi hata miaka ishirini na zaidi pole sana ushauri wangu ndio huo ukipenda chukua usipopenda basi uwamuzi wako goodluck

Bila jina alisema ...

Maji yakishamwagika hayazoleki jikubali kwamba hukuwa mwaminifu kwa mkeo.ukimwi sio mwisho wa maisha ondoa hofu jikubali,mwombe mke wako mkapime afya zenu ili wote mjitambue kama yeye kisha pata maambukiziau la ili mfuate masharti.maumbile ya mwanamke kupata maambuki ni rahisi sana kuliko wanaume kutokana na maumbile yetu.fanya haraka akapime mwenzi wako

Bila jina alisema ...

kaka pole sana kwa lililo kukuta ila jua wewe c wakwanza na wala si wamwisho kupata maambukizi, chakufanya mwombe mkeo ,mkapime alafu majibu yakishatoka uyo doctor atawashauri vema tu. na tunaomba utuambie what next

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom