Jumatano, Juni 26, 2013

KOSA LANGU NI LIPI...? SURA ....YA ....10......



 ILIPOISHIA
Baadaye Mama Robert alijiandaa na kwenda kumpokea mume wake ilikuwa ni furaha isiyo na kifani, Mama Robert alimkaribisha mume wake pamoja na watoto wake kwa furaha na baadaye walielekea nyumbani. Ambapo moja kwa moja walienda kukoga kwanza na baadaye  walienda  mezani kupata chakula cha jioni. Wakati huo Joyce alikuwa  amejipumzisha chumbani kwake kwa muda mrefu hivyo hakuonana na wageni.NINI KITAENDELEA USIKOSE ....SURA YA....10
 
INAPOENDELEA
 
Baadaye Mama Robert aliamua kumuita Joyce ili amtambulishe  kwa mume na watoto wake “Joyce mwanangu” aliita Mama  Robert Joyce akiwa chumbani aliitika  huku akinyanyuka na kuelekea sebuleni “Abee mama” Alipofika kwa mshangao Yule baba alikuwa kama amemfananisha Joyce kisha akauliza “Huyu binti ni nani mama Robert?”  Aliuliza lakini kabla hajajibiwa Joyce aliwakatisha kwa kumsalimia “Shikamoo Baba” Aliitika “Marahaba” Mama Robert akaanza kumtambulisha, "Mume wangu huyu binti anaitwa Joyce ni msichana wa kazi hapa nyumbani ni binti mpole na anajua sana kufanya kazi” Baba Robert akasema “Alaa karibu sana binti karibu uketi” Joyce alijisogeza taratibu na kujumuika pamoja nao.

  Baba Robert aliendelea na maswali  “ Joyce wewe umetokea wapi? na wazazi wako wanaishi wapi”? Joyce akamjibu mimi nilikuwa nikiishi hapahapa Dar es salaam, sina wazazi kwani walishafariki” alisema Joyce kwa sauti ya upole. “Pole sana binti baba yako alikuwa anaitwa nani na inamaana hauna ndugu”? Aliuliza maswali mengi kwa wakati mmoja. Joyce alimjibu na kusema “ Baba yangu alikuwa anaitwa Ndesanjo Kimaro, kuhusu ndugu sikuwahi......” Kabla hajamalizia kuzungumza Baba Robert alimkatisha "Unasema Ndesanjo Kimaro?” Wewe ni mtoto wa Ndesanjo alikuwa anafanya biashara ya bidhaa za kilimo” Joyce alishangaa kuona Baba Robert anamfahamu baba yake kwani ni kweli baba yake alikuwa akijishughulisha na biashara ya bidhaa za kilimo, akasema “Ndiyo baba yangu alikuwa anafanya biashara hiyo” 

"Mungu wangu kumbe Ndesanjo alifariki Mama Robert huyu mtoto ni ndugu yangu kabisa. Ndesanjo ni mdogo wangu tumezaliwa na Baba mmoja lakini hatukuwasiliana ni muda mrefu tokea nilipokuwa nje ya nchi kikazi. Siamini ninachokisikia, lakini pia si alikuwa na watoto wawili na mwingine wa kiume, yuko wapi mdogo wako?”  Joyce aliinama chini kwa uchungu huku machozi yakimtoka akasema “Baba na Mama walifariki kwa ajali ya gari, na Mdogo wangu amefariki alikuwa anaumwa sikuwa na pesa za kumpeleka Hospitali” Baba Robert alihuzunika sana baada ya Joyce kumsimulia kila kitu, aliahidi kumsaidia Joyce katika maisha yake yote.


Maisha ya Joyce yalibadilika sasa alikutana na ndugu zake aliishi kwa furaha na walimpenda sana. Kuna wakati Joyce alikuwa akiwaza “Yalaiti mdogo wangu angelikuwa hai. Tungeishi pamoja haya maisha ya furaha” Siku zilienda  baadaye Yule baba yake mkubwa aliamua kumpatia kazi  Joyce katika duka lake la vifaa vya ujenzi na kumlipa mshahara kila mwisho wa  mwezi.

Maisha yaliendelea Joyce alipendeza sana. Kwani alikuwa ni msichana mrembo ambaye kila mwanamume aliyekuwa akimuona alivutiwa naye, Joyce alifahamiana na watu mbalimbali na wengi walikuwa wakikutana pale dukani. Ilipita miaka miwili tokea maisha ya Joyce yabadilike na alisahau matatizo aliyokutana nayo kipindi cha nyuma. Ilifikia kipindi akapata  rafiki ambaye alikuwa anaitwa Fredy, walikuwa ni marafiki sana.Baadaye walifikia hatua ya kuwa wapenzi.

 Siku moja Fredy  alimfuata Joyce dukani ilikuwa ni jioni mida ambayo Joyce alikuwa akifunga duka “Habari mpenzi naomba leo tutoke kuna kitu  cha muhimu nataka tuongee” Joyce alimjibu akisema “Mmmh Fredy kitu gani hicho mpenzi leo sitaki kuchelewa kurudi nyumbani si unajua Baba na mama ni wakali hawapendi nichelewe” “Hapana yaani haitachukua muda mrefu nitakurudisha mapema” Alisema Fredi “Basi hakuna tatizo ngoja nimalizie kazi haraka, nifunge duka tuondoke” Fredy aliondoka na kwenda kumsubiriJoyce katika gari lake aina ya Rav 4. 

 
Baadaye Joyce alimaliza kazi zake na Kumfuata mpenzi wake kisha waliondoka na kuelekea maeneo ya Posta, Walitafuta sehemu tulivu maeneo ya City Garden kwa ajili ya mazungumzo walikaa pale huku wakiendelea kupata vinywaji Fredy alianza kwa kusema  “Joyce mpenzi unajua tumekuwa katika mahusiano kwa muda mrefu natamani sasa uwe mama wa watoto wangu, nadhani sasa ni wakati mzuri tufunge pingu za maisha.” Alisema Fredy, 

 Joyce aliyekuwa anakunywa Juisi kwa wakati huo alishusha glasi yake mezani. Kisha  alimkumbatia mpenzi wake kwa furaha “ Jamani Fredy nimefurahi kusikia hivyo, nami nakupenda sana nipo tayari maisha yangu niishi na wewe  katika shida na raha nakupenda sana mpenzi”  Basi ilikuwa ni furaha, waliendelea kuzungumza na baadaye waliondoka. Fredy alimrudisha Joyce nyumbani kwao wakiwa njiani Fredy alitoa ahadi ya kwenda kujitambulisha rasmi kwa kina Joyce mapema siku za usoni. JE NINI KITAENDELEA......USIKOSE SURA  YA......11

Maoni 2 :

Bila jina alisema ...

Daaaah! kweli hakuna marefu yasiyokuwa na ncha pia ukipata majaribu ukavumilia lazima ushinde tu. afadhali mungu kamkumbuka joyce kafanikiwa kukutana na ndugu yake. mola awe naye cku zote za maisha yake

Bila jina alisema ...

kwann hanafanya haraka joyce jmn?badala ya kilio ss furaha bora.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom