Jumamosi, Juni 22, 2013

KOSA LANGU NI LIPI...? SURA YA .....9.......



 ILIPOISHIA
Ilikuwa ni majira ya  saa moja za jioni. Joyce alilia na kumuomba sana Maliki asiwafukuze lakini hakuswasikiliza, kwani yule mwanamke aliyekuja naye alikuwa hataki kina Joyce waendelee kuishi pale, hivyo hawakuwa na namna nyingine zaidi ya kuondoka. Huku wakifukuzwa kwa maneno ya kashfa.Bila  ya kujua wapi wanaenda walitembea huku na kule ili kutafuta sehemu ya kujipumzisha kwa usiku huo. JE NINI KITAENDELEA USIKOSE SURA YA....9....

 INAPOENDELEA


Walirudi katika maisha ya mitaani ambayo yalikuwa ni maisha ya shida sana. Kwasababu walikuwa hawana chochote zaidi ya kuomba huku na kule. Siku moja kutokana na kuishi maisha ya tabu  James alianza kuumwa homa. Lakini dada yake alikuwa hana pesa ya kununua dawa. Ilimbidi aombe watu ili wamsaidie, alipata msaada wa kununua dawa,  lakini siku zilivyozidi kwenda hali ya James ilizidi kuwa mbaya.  kutokana na hali halisi ya maisha Joyce alikuwa kama amechanganyikiwa akimtizama mdogo wake anavyoumwa “Nitafanya nini mimi, nimejaribu kutafuta pesa bila mafanikio na James anaumwa sana” Joyce ilimbidi aanze kujiuza ili apate pesa za kumpeleka mdogo wake Hospitalini. Alijiingiza katika biashara ya ukahaba ili aweze kupata pesa za mahitaji mbalimbali.

Wakati mwingine iliwabidi walale njaa kutokana na hali halisi ya maisha. Akiwa anaendelea na biashara hiyo alikutana na changamoto nyingi sana. Siku moja alikutana na mwanaume mmoja ambaye alionekana kuwa na umbo kubwa mithili ya mmbeba vyuma, alimchukua na kumuahidi kuwa angemlipa kiasi kikubwa cha fedha. Walipofika chumbani yule mwanaume alimtaka Joyce afanye naye mapenzi kinyume na maumbile lakini Joyce alikuwa akikataa “Sitaki, naomba uniache, unaniumiza jamani, sitaki siwezi mimi” Alikuwa akilalamika Joyce huku akijitoa mikononi mwa yule mwanaume bila mafanikio. Kwani aliambulia kipigo kikali sana, yule mwanaume alimpiga Joyce na kumlazimisha kufanya naye mapenzi kwa nguvu.Joyce alilia sana kwa uchungu. Baadaye yule kaka aliondoka bila hata ya kumlipa pesa yoyote na Joyce alibaki akilia kutokana na  maumivu makali sana aliyokuwa akiyasikia.

  Pesa alizokuwa anapata Joyce zilikuwa hazitoshi kuwasaidia na huku  hali ya James haikuwa nzuri hatimaye alifariki Dunia. ni siku ambayo Joyce alilia kwa uchungu bila ya kujua nani atamsaidia katika maisha yake. Alisaidiwa na watu mbalimbali wa mitaani katika mazishi ya mdogo wake  na baadaye alibaki pekee bila kujua ataenda kwa nani ili aweze kumsaidia.
  

Siku zilienda Huku Joyce  akiwa amekata tamaa ya maisha. Baadaye aliamua kutafuta kazi za ndani ili aweze kujikimu katika maisha. Alihangaika sana  huku na kule bila ya mafanikioBaadaye  alifanikiwa kupata kazi katika nyumba ya Mama mmoja aliyejulikana kwa jina la Mama Robert.  alimuonea sana huruma baada ya kumueleza kila kitu kuhusu mkasa mzima wa maisha yake basi alianza rasmi kufanya kazi katika nyumba hiyo.

 Ambapo  kwa wakati huo mume wake na Mama Robert alikuwa amesafiri, pamoja na watoto wake wawili.  Zilipita kama wiki mbili Joyce akiwa anaendelea na kazi bila matatizo yoyote "Mwanangu unafanya kazi vizuri sana lakini pia uwe unapumzika siyo lazima ufanye kazi zote kwa mara moja" Alisema Mama Robert huku akimsisitiza Joyce awe anapumzika kwani Joyce alikuwa akifanya kazi sana bila ya kuchoka. Kesho yake ilikuwa ni siku ambayo  Baba Robert ndiyo anarudi kutoka safari.

  Kesho yake  Mama Robert aliandaa chakula kizuri akishirikiana na Joyce. Yalikuwa ni maandalizi ya kumpokea mume wake pamoja na watoto wake. Waliandaa kila kitu mazingira ya nyumbani yaliwekwa katika hali ya usafi. Baadaye Mama Robert alijiandaa na kwenda kumpokea mume wake ilikuwa ni furaha isiyo na kifani, Mama Robert alimkaribisha mume wake pamoja na watoto wake kwa furaha na baadaye walielekea nyumbani. Ambapo moja kwa moja walienda kukoga kwanza na baadaye  walienda  mezani kupata chakula cha jioni. Wakati huo Joyce alikuwa  amejipumzisha chumbani kwake kwa muda mrefu hivyo hakuonana na wageni.NINI KITAENDELEA USIKOSE ....SURA YA....10


Maoni 2 :

Bila jina alisema ...

Mhhhhh uyo baba Robert nawasi was naye.

Bila jina alisema ...

Mungu msaidie, kapita kwingi

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom