Jumamosi, Juni 08, 2013

SIMULIZI ....KOSA LANGU NI NINI....... SURA YA ....5........


ILIPOISHIA
Baada ya muda kupita mnamo saa sita usiku Joyce alikuwa bado amejilaza sebuleni na mlango wa sebuleni ulikuwa haujafungwa, Maliki alirudi usiku huo aliingia moja kwa moja  na kumkuta Joyce akiwa amelala kwenye kochi alisimama kwa muda pale mlangoni huku akimtazama Joyce kwa umakini na moyoni mwake akisema "mmmh huyu mtoto nampenda sana embu tizama alivyolala kama Malaika, mzuri sana huyu binti namtamani" JE NINI KITAENDELEA USIKOSE SURA YA....5...

INAPOENDELEA 
Akiwa anawaza huku anasogea taratibu katika kochi alilokuwa  amelala.Joyce alikuwa amevalia gauni fupi, na kwa namna alivyokuwa amelala sehemu ya paja ilikuwa inaonekana basi Maliki alipofika alianza kumshika pajani Joyce huku akimpapasa taratibu Joyce alishtuka kutoka usingizini "Aaah jamani kaka Maliki umenishtua" .

Maliki alinyanyua mkono wake wa kulia na kumshika Joyce mikono yake miwili "Joyce mpenzi kwa nini unanitesa hivi si unajua kwa kiasi gani mimi nakupenda nahitaji penzi lako nakuomba unikubalie naahidi sintokuumiza nakupenda sana". Alisisitiza Maliki huku akimpapasa Joyce viganja vya mikono yake.
 Joyce aliyekuwa amejiinamia kwa  aibu alisema "Kaka Maliki mimi naogopa haiwezekani mimi bado mdogo,wewe niache mimi siwezi naomba unisamehe kama kuna jambo nimekukosea naomba uniache usinifanyie hivi mimi sitaki". Maliki aliyekuwa anaonekana amelegea macho huku akimtazama Joyce kwa matamanio  alimkumbatia Joyce kwa nguvu  "nikupe nini mpenzi nakupenda nikubalie ombi langu".

 Joyce huku akiwa  anatetemeka alijaribu kujivuta ili ajitoe mikononi mwa Maliki bila mafanikio. Akiwa anaendelea kujaribu kujitoa Maliki aliisogeza midomo yake karibu na midomo ya Joyce, na kuanza kumbusu kwa umakini kabisa aliendelea kumshikilia kwa nguvu baadaye alimbeba na kumpeleka Chumbani ambapo Joyce alibaki akilalamika "Kaka Maliki mimi naogopa naomba uniache unaniumiza" Alisema Joyce ambaye ilikuwa ndiyo mara yake ya kwanza kuwa katika mapenzi.

 Maliki aliyekuwa kama amechanganyikiwa hakumsikiliza aliendelea hadi alipomaliza alichokuwa anakitaka kwa Joyce baada ya kumaliza  akaanza kumbembeleza Joyce aliyekuwa akilia kwa maumivu makali "Pole mpenzi usijali mimi nakupenda Joyce usilie nyamaza mpenzi" Joyce aliendelea kulia baadaye aliondoka huku akichechemea kwa maumivu, alienda kuoga na kurudi chumbani kwake kulala huku moyoni akiwa anawaza "Siamini kama Kaka Maliki amenifanyia  kitendo kibaya hivi,sijui nitoroke na mdogo wangu, mimi siwezi kuishi haya maisha inaniuma sana, na je kama nitatoroka nitaenda wapi? Na sina mtu wa kunisaidia" Aliwaza Joyce huku akiwa analia kwa uchungu.

Wakati Joyce akiwa anaendelea kulia na kuwaza kama atoroke au aendelee kuishi katika nyumba ya Maliki, usingizi ulimpitia na kulala hadi mida ya saa moja asubuhi ambapo mdogo wake alikuja kubisha hodi ili kumuamsha dada yake, kwani ilikuwa siyo kawaida yake kulala hadi muda huo. Siku zote alikuwa akiamka mapema na kufanya kazi za pale nyumbani ikiwemo kumuandalia mdogo wake kifungua kinywa kabla ya kwenda shule.


 Wakati James akiwa anabisha hodi, mwanzoni dada yake hakumsikia aliendelea kugonga  mlango kwa nguvu  baadaye Joyce alimsikia hivyo alinyanyuka taratibu kwa uchovu  na kuelekea kwenye mlango kisha kuufungua. James alimsalimia "shikamoo dada" Joyce aliyekuwa kama bado yupo usingizini alimtazama na macho yake yalikuwa yamevimba kutokana na kulia sana akasema "Marahaba James haujaenda shule?" James alimshangaa dada yake kwa hali aliyokuwa nayo na kusema "Sijaenda bado nilikuwa nakusubiri uniandalie chai,vipi dada unaumwa mbona macho yako yamekuwa ya rangi nyekundu na yamevimba sana"

Joyce alinyamaza kimya kwa muda na kumshika mdogo wake kichwani   na kusema "usijali mdogo wangu kichwa kinaniuma twende nikuandalie chai utachelewa shule" Joyce aliingia jikoni na kuchemsha maji kwenye birika kisha akachukua mkate kwenye kabati na kumuandalia mdogo wake chai ili awahi kwenda shule,baada ya kumaliza kunywa chai James alichukua mkoba wake wa shule na kuondoka huku akimsisitiza dada yake atumie dawa ya kichwa ili asiumwe tena.

Masikini James alikuwa hajui kilichomsibu dada yake. baada ya James kuondoka Joyce alibaki amejiinamia huku akiwaza "Jamani maisha gani haya,Kaka Maliki amenifanyia unyama nasikia maumivu makali sana, na  kama nikiondoka James nani atamsomesha,  sina budi kuendelea kuishi hapa napenda sana mdogo wangu asome ukizingatia anao uwezo mzuri katika masomo yake, natamani sana afikie malengo yake. yalaiti wazazi wetu wangekuwepo.Yaani kina Mama Ngonyani na majirani walitutenga na kutuacha tukiteseka, pesa yenyewe sina ya kulipia kodi hata chakula nitaenda wapi?".

 Joyce akiwa anaendelea kufikiria mara Maliki alitoka chumbani kwake, na kumuona Joyce akiwa amekaa kwenye kochi huku akiwa ameweka mkono wake wa kulia shavuni. Joyce alikuwa hajamuona, Maliki alitembea kwa kunyata taratibu na alipofika karibu alimshika mkono, Joyce alishtuka na kusema "Mama yangu!" Maliki alicheka kidogo na kusema "mmmh mtoto mbona unaogopa sana, umeamkaje mpenzi wangu"

 Joyce alimwangalia Maliki kwa muda huku akionyesha uso uliojaa hasira na woga "Shikamoo kaka Maliki" akamjibu "Acha hizo Joyce mimi nakupenda haina haja ya kunisalimia wewe ni mpenzi wangu"Huku akijisogeza taratibu na kumshika begani" Joyce akainama chini kimya bila kujibu chochote huku Maliki akiendelea kuchombeza "Mmh mtoto mtamu wewe jana nilifaidi sana,sintokuacha kipenzi changu na kama kuna kitu chochote unataka usisite kuniambia nipo kwa ajili yako". Joyce alimwangalia Maliki nakusema "lakini kaka Maliki mimi sipendi unavyonifanyia" kabla hajamaliza Maliki alimkatisha  "Najua unaogopa kwasababu haujazoea huu mchezo ni mzuri sana ipo siku utaona raha yake" Niandalie chai basi mpenzi wangu kwani leo hata kazini siendi nataka unipe raha zaidi ya jana"Alisema Maliki huku akielekea mezani kunywa chai. ..JE NINI KITAENDELEA ....USIKOSE....SURA YA .....6.....

Maoni 5 :

Bila jina alisema ...

Uwiiiiii majanga hya,jmn.joy.pole mpz ndo ukubwa namaisha

Bila jina alisema ...

Mmmhh! Jamani inatia huruma lkn.... mmmh

Unknown alisema ...

dah adela umenigusa sana, fanya haraka basi nipate no 6 maana story tamu sana. Vp kuhusu kitabu?

ADELA KAVISHE alisema ...

asanteni sana wadau tuendelee kuwa pamoja muendelezo ni siku ya jumatano, na kuhusu kitabu mdau nitatoa taarifa hivi karibuni

emuthree alisema ...

Kazi nzuri mpendwa, tupo pamoja, nashukuru kuwa umeweza, na unanipa moyo kuwa huenda nami siku moja nitaweza

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom