Jumamosi, Julai 13, 2013

KOSA LANGU NI LIPI...? SEHEMU YA ...15......



 ILIPOISHIA
“Wewe una kichaa mtoto si wa kwako tena naomba uondoke katika nyumba yangu kabla sijakuitia Polisi” Sukari akacheka kidogo na kusema “Halafu ukiwaita hao Polisi utakuwa umenisaidia sana, mimi naondoka lakini nitarudi hadi nihakikishe nampata mwanangu”....USIKOSE SEHEMU YA ....15......


INAPOENDELEA
Sukari aliondoka na kumuacha Joyce akiwa kama amechanganyikiwa  “Mungu wangu sijui nitafanyaje Fredy akigundua ataniua, na mambo yanazidi kuwa mabaya. Halafu leo jioni anarudi kutoka safari, sijui itakuwaje, naogopa sana Mungu wangu nisaidie.Hivi ni kwaninini Lina ameamua kunisaliti jamani yaani  amempa Sukari namba yangu ya simu? Sijui itakuwaje, yaani nimekwisha” Aliwaza Joyce.

Jioni ya siku hiyo Fredy alirudi kutoka safari. Alimkuta Joyce akiwa amekaa sebuleni “Mke wangu kipenzi habari za  masiku” Joyce kwa furaha alimsogelea Fredy na kumkumbatia “Karibu mume wangu, pole na uchovu wa safari,ni matumaini yangu umekuja na habari njema za huko” Fredy  huku akionyesha tabasamu pana katika paji la uso wake akasema  “ Habari za huko ni nzuri, lakini si kwema kuna taarifa nimezipata zinasikitisha sana” Joyce alishtuka akifikiri Fredy ameshaambiwa ukweli kuhuhusu mtoto wake.  Alishusha pumzi huku akionekana kujiumauma na sauti iliyojaa kigugumizi akasema “ Umesema kuna nini? Kwanini? Ilikuwaje?” Fredy alishangaa kumuona Joyce katika hali ile  "Vipi mama James mbona umeshtuka sana" Alihoji Fredy.

 "Hapana nilikuwa nataka kufahamu kuna nini? Eeeh kuna nini?" Alisema Joyce huku akiwa kama hajiamini  Fredy aliguna kidogo "Mmh wewe utakuwa una matatizo, sijawahi kukuona katika hali kama hiyo,habari nilizozipata za kusikitisha ni kuhusu  rafiki yangu yangu kipenzi ambaye tulipotezana kitambo,  amekamatwa na polisi, na kutokana na kutaka kuwashabulia polisi, basi wamempiga sana kabla ya kufikishwa kituoni na sasa ninavyozungumza nasikia hali yake ni mbaya" Joyce aliyekuwa akimsikiliza kwa umakini huku akitikisa kichwa akasema "Maskini kwani amefanya kosa gani?" "Huyu jamaa   kumbe alikuwa anajihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya  kwa muda mrefu sana, kama unavyojua siku zote  siku za mwizi ni arobaini, hivyo polisi walipokwenda kumkamata kulikuwa na malumbano, na jamaa alikuwa anamiliki Bastola kinyume cha sheria, yaani ni kisa kirefu kwakweli”.


 Joyce kusikia hivyo alishusha pumzi na kusema “Daah, ni jambo la hatari sana, unajua huku mitaani unaweza kumuona mtu hana kazi yoyote, lakini anamiliki gari la kifahari na kufanya starehe za hapa na pale. Kumbe yawezekana akawa anafanya biashara haramu ya kuuza madawa ya kulevya, halafu kwa kiasi kikubwa vijana ndiyo waathirika katika biashara hii kwani wao ndiyo wanatumiwa na vigogo. Inasikitisha sana, kwahiyo anaendeleaje huyo rafiki yako."

Fredy alimtizama mke wake na kusema“Hapa nilipo nataka kesho asubuhi na mapema niende kumuona, tunaweza kwenda pamoja” Joyce akamjibu “Bila shaka mume wangu tutaenda pamoja” baadaye Fredy aliingia ndani na kukoga kisha kupata chakula cha usiku na kwa upande wa Joyce alikuwa hana raha muda wote alikuwa ni mtu aliyejaa wasiwasi.

Kesho yake asubuhi na mapema Joyce aliamka na kuandaa uji kwaajili ya kwenda kumpelekea mgonjwa. Baadaye awalijiandaa na kuanza safari ya kwenda hospitali.  Walipofika Hospitalini waliulizia mahali alipokuwa mgonjwa  na moja kwa moja walielekea katika wodi aliyolazwa mgonjwa,   walipofika mgonjwa alikuwa ndiyo anaamka kutoka usingizini, Akiwa anajaribu kufumbua macho yake taratibu alijikuta akimtizama Joyce.Alishtuka sana baada ya kumuona Joyce  kwa sauti ya unyonge akasema “Joyce Joyce ni wewe au nipo ndotoni,  siamini macho yangu” Joyce alimuangalia kwa makini, kwani alikuwa ameumia sana sehemu za usoni kwahiyo ilikuwa ni vigumu kumtambua yule mgonjwa alikuwa ni nani. Baada ya kumtizama kama dakika moja   “Hee! Ni wewe Maliki,Mungu wangu ama kweli milima haikutani binadamu hukutana” Fredy alibaki anashangaa kwani alikuwa hajui nini kinaendelea kati ya Joyce na Maliki akasema
“Inamaana mnafahamiana”.

 Maliki aliyekuwa kitandani aliongea kwa uchungu akisema “Joyce nimekutafuta ni muda mrefu sana bila mafanikio, naomba unisamehe kwa yote niliyokutendea na Mungu anisamehe pia. Najuta kwa yote niliyokutendea nilikunyanyasa bila ya huruma naomba unisamehe. Hapa nilipo sijui kama nitapona naumwa sana na maisha yangu nitakufa hata mtoto sina, nahisi Mungu amenipa adahabu kali, nakumbuka ulivyokuwa ukipata ujauzito nakulazimisha utoe mimba,  nisamehe Joyce niombee msamaha na kwa mdogo wako pia” Aliongea kwa uchungu maneno mengi bila kupumzika huku machozi yakimbubujika mithili ya mtu aliyemwagiwa maji” 

Joyce aliyekuwa amesimama,pembezoni mwa kitanda alichokuwa amelazwa mgonjwa  alisogea karibu na kusema "Nilishakusamehe tokea zamani Maliki, na kuhusu  mdogo wangu alifariki kutokana na shida tulizopata mitaani bila ya msaada wowote, baada ya wewe kutufukuza nyumbani kwako, mimi nimekusamehe” Fredy alishindwa kuelewa kinachoendelea alihisi kama maigizo kwani Joyce hakuwahi kumuambia kuhusu uhusiano wake na Maliki.

Baada ya Joyce kumuambia Maliki kuwa amemsamehe Maliki akasema “Asante sana Joyce Mungu akubariki, Fredy huyu mwanamke aliwahi kuwa mchumba wangu, zamani kidogo  nilimkosea sana nashukuru Mungu leo nimekutana naye na kupata nafasi ya kuomba msamaha.” Alisema Maliki huku akimuangalia Joyce kwa aibu"  Fredy  alimwangalia Joyce  na kisha kumtizama Maliki " Ohhh inaelekea mna historia ndefu kidogo, vipi hali yako lakini" Aliuliza Fredy kwa sauti iliyokosa uchangamfu Maliki hali yake haikuwa nzuri hivyo ilikuwa si rahisi Fredy kuhoji maswali mengi basi waliendelea na mazungumzo na baadaye waliondoka.

 Walipofika nyumbani ilimbidi Joyce amsimulie mume wake maisha yake yalivyokuwa kipindi alivyokuwa na Maliki. Fredy alimwambia asimfiche chochote juu ya maisha yake kwani kitendo cha kumficha kinampa wasiwasi katika mapenzi yao "Hakuna kitu kibaya na nichokichukia kama uongo hususani kwa mtu ninayempenda na kumuamini naomba usinifiche chochote kuhusu maisha yako yalivyokuwa kipindi cha nyuma"Alisema Fredy huku akimkazia macho Joyce aliyekuwa ameinama kwa aibu. "Naomba unisamehe mume wangu, nilishindwa kukuambia  kutokana na kwamba sikupenda kabisa kukumbuka mateso niliyoyapata kipindi cha nyuma, nisamehe mume wangu, nakupenda sana kamwe siwezi kukuficha jambo lolote lile. JE NINI ....KITAENDELEA ....USIKOSE....SEHEMU ....YA .....16...



 
 
 

Maoni 2 :

Bila jina alisema ...

Cna lakusema leo.Malik majuto ni mjukuu

Bila jina alisema ...

Kweli wa2 walinena kuwa "malipo ni hapa hapa duniani" maliki kapata amepata alichotaka

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom