Jumatano, Julai 17, 2013

SIMULIZI KOSA LANGU NI LIPI...? SEHEMU YA ......16........



 ILIPOISHIA
"Naomba unisamehe mume wangu, nilishindwa kukuambia  kutokana na kwamba sikupenda kabisa kukumbuka mateso niliyoyapata kipindi cha nyuma, nisamehe mume wangu, nakupenda sana kamwe siwezi kukuficha jambo lolote lile. JE NINI ....KITAENDELEA ....USIKOSE....SEHEMU ....YA .....16...

INAPOENDELEA
Zilipita kama siku mbili Joyce akiwa bado anasumbuliwa na Sukari kuhusu mtoto. Alikuwa na wasiwasi sana muda wote alikuwa hana raha. Huko hospitalini  hali ya mgonjwa haikuwa nzuri , hatimaye Maliki alifariki baada ya kuugua sana.Maisha yaliendelea siku moja Joyce aliamua kumpigia simu Lina ili amsaidie kuhusu matatizo aliyonayo lakini alipiga simu iliita bila ya mafanikio, na hata alipojaribu tena baadaye hakupokea, "Eeeh Mungu yaani huyu Lina kweli ananifanyia hivi angalau angepokea simu yangu basi" alisema Joyce huku akiinama chini na kutikisa kichwa kwa masikitiko mambo yalizidi kuwa mabaya kwa upande wa Joyce ambaye muda wote alikuwa anawaza nini kitatokea endapo mume wake akigundua mchezo mchafu alioufanya.

 Fredy alikuwa akihisi mke wake ana matatizo kutokana na namna ambavyo alikuwa akionyesha wasiwasi katika kila jambo akiwa kazini Fredy aliwaza “Hivi siku hizi mke wangu ana matatizo gani yaani simuelewi amekuwa mtu wa kuishi kwa wasiwasi sana. Leo nikirudi nyumbani itabidi nimuulize hadi aniambie nini kinachomsibu” Aliwaza  Fredy na baadaye alipotoka kazini ilikuwa mida ya saa moja jioni alifika nyumbani na kuingia bila ya kugonga mlango.

 Joyce alishtuka kumuona “Mama yangu umenishtua sana Fredy” Fredy alishangaa kumuona namna ambavyo Joyce alivyoshtuka na kusema “Sasa nimekushtua na kitu gani halafu wewe una matatizo sana embu keti hapo tuzungumze” Alihamaki Fredy huku akimuangalia kwa umakini mke wake Joyce taratibu alijisogeza na kuketi huku akisema “Yaani wewe huoni kama umenishtua umeingia bila ya kugonga mlango halafu unaniambia mimi nina matatizo sawa bwana” Alilalamika Joyce Fredy akamuuliza “Unajua kinachonishangaza ni mabadiliko ya tabia yako umekuwa mtu wamashaka mashaka sana siku hizi vipi una matatizo gani? Au kuna kitu unanificha”.


 Joyce alimtazama Fredy kwa macho ya upole na kusema “Nina mashaka? Hapana mume wangu mbona mimi nipo sawa sina matatizo yoyote” Fredy akacheka kidogo na kusema “Wewe ndiye unajiona uko sawa mimi nakujua vizuri sana mke wangu. Huwezi kunidanganya kuwa hauna matatizo haya hebu niambie ukweli sitaki unifiche kitu kama kuna tatizo kuwa muwazi” Joyce aliendelea kudanganya na kusema “mimi sina matatizo niko sawa jamani mume wangu kama kuna tatizo kwanini nikufiche” Fredy aliguna kidogo na kusema “Sawa kama hakuna tatizo mimi naingia ndani niandalie maji ya kuoga” aliongea huku akiwa anaelekea chumbani.

Joyce alibaki akiwa na wasiwasi na kuelekea kumuandalia maji ya kuoga mume wake. Kwa upande wa Sukari alipanga namna ya kuja kumuumbua Joyce kama ataendelea kukaidi kumtambulisha kwa mtoto wake. "Yaani haiwezekani kabisa, mimi mwanaume mzima na akili zangu, mtoto wangu analelewa na baba mwingine, hivi huyu Joyce ananionaje, siwezi kukubali hata kidogo lazima nimchukue mtoto wangu. yaani wanawake wengine ni watu wa ajabu sana. Aliwaza Sukari huku akionekana kuwa na hasira nyingi.

 Siku hiyo ilikuwa ni siku ya Jumatatu ambapo Joyce alikuwa katika shughuli zake za kibiashara na mume wake Fredy alikuwa nyumbani kwani siku hiyo alikuwa amewahi sana kutoka kazini ilikuwa ni mida ya saa nane za mchana Sukari alifika nyumbani Kwa Joyce na kugonga geti.

 Mlinzi wa getini alifungua na kumuona Sukari  “Ni wewe tena, umefuata nini?  hakuna kuingia hapa, ishia hapohapo. Mama mwenye  nyumba alisema hata siku moja nisikufungulie geti” Alisema mlinzi kwa sauti kali,  akiwa anazungumza Fredy alimsikia kwasababu alikuwa maeneo ya karibu na kwenye geti akauliza “Kuna nini hapo?  Nani unabishana naye, mkaribishe ndani” mlinzi akamjibu “Huyu kijana kuna siku alikuja walikuwa wakigombana na Mama kwahiyo Mama alisema hata sikumoja nisimfungulie geti, vinginevyo atanifukuza kazi”.

 Fredy alishangaa kusikia hivyo na kusema “Embu mkaribishe ndani”  Sukari ambaye muda wote alikuwa amenyamaza kimya aliingia ndani Fredy alimtizama huku akijiuliza maswali na nafsi yake "Mbona mimi huyu mtu simfahamu, na anamfahamu vipi mke wangu." Aliwaza na kumsalimia Sukari "Habari  yako, karibu sana, sijui ulikuwa na shida gani" Aliuliza Fredy huku Sukari akiwa anamtizama bila ya kuzungumza chochote. Je nini kitaendelea usikose ...SEHEMU ....YA 17.....

Maoni 6 :

suzy alisema ...

Ehee mungu naomba waende wakapime. DNA akute si mtt wake akome. Kiherehere cha kumsumbua Joyce na. Lina haaibike

Bila jina alisema ...

mhhhhhhhhhhh am sure sukari hataumbuka,mna naic uyo mtto hajafanana nae,lina nae hatkufa mdomo wazi.

Bila jina alisema ...

Daaaaaaah! siamini macho yangu, hapo siongei nakaa pembeni kusikilizia mchezo unavyoendelea.

Bila jina alisema ...

He! he! he! he! he! he! he! ukisikia kufa kwa nyani miti yote huteleza ndo hapo, na hapo lazima miti yote ya joyce lzm iteleze tu.

Bila jina alisema ...

"Assalale mtume wangu! hapo kapatikana"

Bila jina alisema ...

"Yesu na maria,! mungu na mtume!" udanganyifu wake umefikia mwisho. akumbuke kuwa uongo haufai katika ndoa.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom