Jumapili, Agosti 25, 2013

KWAKO KIJANA SOMA STORY HII FUPI UPATE KITU.....


Siku moja punda wa mkulima alianguka
ndani ya kisima. Mnyama huyo alipiga
kelele kinyonge kwa masaa kadhaa wakati
mkulima akijaribu kufikiri nini cha kufanya.
Hatimaye, aliamua kwakuwa punda wake
alikuwa mzee, na pia kisima hicho kilihitaji
kufunikwa juu, Akaona hapakuwa na haja
ya kumtoa.
Akaita majirani zake wote waje kumsaidia.
Wao wote wakachukua makoleo na kuanza
kuchota taka kwa koleo na kuzitupia ndani
ya kisima. Mara ya kwanza, punda
aligundua nini kilikuwakinatokea akapiga
kelele kwa nguvu. Basi, ikawashanganza
wale watu punda aliponyamaza ghafla!
Baada ya kutupa taka kadhaa kwenye hicho
kisima. Huyo mkulima alishangazwa na kile
alichokiona. Kwamba kila koleo la taka
lililorushwa juu ya mgongo wa punda,
punda alikuwa akifanya kitu cha
kushangaza. Alikuwa akijitikisa ili taka
zimwagike chini huku akipiga hatua moja
kuja juu.
Kadri mkulima na majirani walivyoendelea
kutupa uchafu kwa koleo juu ya punda yule,
alizidi kutikisa mgongo wake na kupiga
hatua moja kuja juu. Muda mfupi baadae,
kila mtu alishangaa jinsi punda alivyozidi
kutokeza ndani ya kisima na kuja juu.

FUNZO:
Maisha yatakutupia kila aina ya uchafu. Ili
utoke nje ya kisima wahitaji kujitikisa na
kuchukua hatua moja juu. Kila tatizo
ulilonalo, ni jiwe la kukuwezesha kukanyaga
na kupiga hatua kuja juu. Tunaweza kutoka
nje ya kisima kirefu kwa kuongeza bidii ya
kupiga hatua moja kuja juu bila kuacha na
kutokata tamaa kamwe.

Tikisa titikisa
uchafu mbali na kuchukua hatua kuja juu.
Kumbuka kanuni 5 rahisi ili uwe na furaha:
1. Weka huru moyo wako mbali na chuki -
Samehe.
2. Weka huru akili yako mbali na wasiwasi -
Wengi hushindwa kabisa kipengele hiki.
3.Tosheka / rizika na ulichonacho.
4. Toa zaidi.
5. Tarajia vichache kutoka kwa watu lakini
zaidi kutoka kwako mwenyewe.

MSHUKURU MWENYEZI MUNGU KWA KILA
JAMBO....

Maoni 3 :

Unknown alisema ...

Neno!

Unknown alisema ...

Neno

Unknown alisema ...

Hii hapa safi sana. Ni wewe uliye tunga ili?
Hendekea na kazi hii bora.
Pat X2 Lion

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom