Jumatatu, Septemba 30, 2013

SIMULIZI YA KOSA LANGU NI LIPI SEHEMU YA 19



ILIPOISHIA
Joyce alikuwa katika wakati mgumu sana, akiwa Hoteli aliwaza sana  “Eeeh Mungu naomba unisaidie, nisamehe kosa langu, sijui nitafanyaje, yaani nahisi kuchanganyikiwa, nyumbani wakigundua baba mkubwa na mama watanifikiriaje najuta sana kukubali ushauri wa Lina. Hapa nilipo nina nina ujauzito wa Fredy, yalaiti ningevuta subira kipindi kile yote haya yasingetokea.Sasa maji yameshamwagika na hayazoleki. nimeharibu kila kitu na Fredy hanitaki tena. Sijui nitaificha wapi sura yangu.eeh Mungu nisaidie" aliendelea kuwaza Joyce huku machozi yakimtoka.JE NINI KITAENDELEA...USIKOSE... SEHEMU YA  18. 

INAPOENDELEA         
Fredy aliamua kwenda nyumbani kwa walezi wa Joyce na kuwaeleza hali halisi kuhusiana na  yaliyotokea  alikuwa akiendesha gari huku akiwa mwingi wa mawazo “Huyu mwanamke ameniaibisha sana sikuwahi kutegemea kama ana tabia mbaya kiasi hiki ni vyema nikawafahamishe na wazazi wake ili wajue nimemfukuza  binti yao”  Alikuwa akiwaza huku akiwa anaendesha gari kwa kasi  bado kidogo asababishe ajali baada ya kumkosakosa  jamaa mmoja dereva taksi “Wewe kijana mpumbavu sana, mlevi nini wewe unaendesha gari ovyo yaani ungenigonga leo ungenilipa gari jipya” Aliongea dereva taksi kwa ukali huku Fredy akijifanya kama hajamuona na kuendelea na safari yake.

Alipofika nyumbani kwa walezi wa Joyce alikaribishwa vizuri sana “Shikamoo mama habari za hapa” “Marahaba Karibu mwanangu habari za nyumbani jamani mbona mmekuwa kimya sana yaani mnashindwa kabisa kuja kutusalimia” Alilalamika Mama Robert “Asante Mama majukumu tu ndiyo yanasabisha kimya kinakuwa kingi” alisema Fredy huku Mama Robert akiwa anaketi katika sofa lilokuwa pembeni yake “Jamani wanangu haiwezekani mkapotea kwa kiasi hicho sisi ni wazazi wenu mnatakiwa kuja kutujulia hali mara kwa mara, haya na huyo mwenzio yuko wapi mbona hamkuongozana?” Aliuliza Mama Robert .

Fredy aliyekuwa amejiinamia kana kwamba kuna kitu anatafakari “Mama kuna jambo ambalo limenifanya nije hapa leo ni vyema na baba angekuwepo ili niweze kuzungumza nanyi wote jambo lenyewe linamuhusu Joyce” Mama Robert  akiwa anamtazama kwa umakini sana Fredy akasema “Mbona unanitisha mwanangu kuna nini kimetokea mwenzio anaumwa au ni nini tena jamani?” Hapana Joyce siyo mgonjwa ila kuna mambo yametokea nadhani ni vyema ukamuita na Baba” Alisisitiza Fredy .


 “Baba Robert ametoka hayupo hapa nyumbani wewe zungumza tu mwanangu hakuna tatizo” Fredy alivuta pumzi na kuanza kumueleza Mama mlezi wa Joyce kila kitu kuhusu Joyce na mambo yote yaliyotokea, wakati wote akiwa anaelezea Mama Robert alikuwa akimtazama kwa umakini huku akiwa ameweka mkono wake katika paji la uso wake.

 “Mungu wangu kweli Joyce anaweza kufanya mambo ya aibu kiasi hiki amepatwa na nini huyu mtoto. Na sasa atakuwa amekwenda wapi na mbona hapa nyumbani hajafika, jamani balaa gani tena hili” Alizungumza mama Robert huku akionyesha kupatwa na hasira kwa kile kilichotokea.Fredy akamjibu”Mama binafsi haya mambo yananiumiza sana akili mimi mwenyewe sikutarajia kama Joyce angeweza kunifanyia mambo yote haya na ukiniuliza ameenda wapi mimi siwezi kujua labda atakuwa amemfuata huyo mwanaume aliyezaa naye inaniuma sana mimi sina lakuongeza nimekuja kutoa taarifa tu kuwa binti yenu sipo naye tena ameniaibisha sana”.

   Mama Robert akainama chini na kuinua uso wake huku akimtazama Fredy “Yaani unajua siamini ninayosikia inamaana .....” Kabla hajamaliza kuzungumza mlangoni kulisikika mtu anabisha hodi

“Nani tena huyu muda huu karibu ingia mlango uko wazi” Aliyekuwa amekuja kwa wakati huo alikuwa ni Joyce alifungua mlango na kuingia alishtuka sana baada ya kumuona Fredy ameketi pale sebuleni alisogea taratibu huku akiwa amejaa wasiwasi mwingi Fredy alimtizama kwa hasira na kunyanyuaka huku akiaga.

 “Mama mimi naondoka nafikiri utakuwa umenielewa” Fredy naomba usiondoke Mume wangu naomba unisikilize mwenzio sikukusudia kukutendea hivyo nakuomba unisikilize” aliongea Joyce huku akipiga magoti na mchozi yakiwa yanamtoka “Nikusikilize kitu gani Joyce sidhani kama mimi na wewe tuna lakuzungumza wewe endelea na maisha yako” Fredy alifungua mlango na kuondoka bila ya kusikiliza chochote na sasa alibaki Joyce na mama yake mlezi.

“Ni aibu gani hii wewe Joyce unajua nashindwa hata kuelewa kwa yote haya yaliyotokea kwanini umeamua kutuaibisha kiasi hiki kweli wewe ni mtu wa kumsaliti mume wako tena umezaa nje yandoa yako huku ukimdanganya mume wako kuwa mtoto ni wa kwake na ni  kwa muda mrefu ukiwa umeficha siri, wewe mtoto si muuaji wewe ni upumbavu gani huu Joyce” Mama Robert alizungumza kwa hasira Joyce akiwa amepiga magoti huku mikono yake ikiwa kichwani .

“Mama naomba unisamehe sikukusudia kufanya hivi ni shetani tu alinipitia na ushauri mbaya wa rafiki yangu nisamehe mama nampenda sana mume wangu. “Funga bakuli lako eti shetani alinipitia na rafiki alikudanganya inamaana wewe hauna akili udanganyike kirahisirahisi tu mjinga sana wewe tena subiri Baba Robert arudi sijui atakufanya nini wewe.

Joyce alibaki kama amemwagiwa maji huku Mama Robert akiendelea kuzungumza "haya na mtoto yuko wapi" huku akiwa amejiinamia chini "Mtoto amemchukua Sukari" kwa mshangao mama Robert akamwambia "Hee! Kweli unajua haya mambo mimi siamini jamani hivii ni kitu gani hasa kilikupelekea kumsaliti mume wako aibu kubwa sana hii sikuwahi kufikiria una tabia za ajabu kiasi hiki".

 Joyce aliinama chini kwa aibu "Mama naomba unisamehe sikukusudia kutenda yote haya ni shetani tu alinipitia nisaidie mama ni wewe pekee unaweza kuwa karibu na mimi" waliendelea kuzungumza baadaye mama Robert alinyanyuka na kuelekea chumbani huku akimtaka Joyce aende chumbani kwake akapumzike. ITAENDELEA  KITABU HIKI KITAWAJIA HIVI KARIBUNI USIKOSE NAKALA YAKO.

Maoni 4 :

Bila jina alisema ...

jaman dada adela mlete kandida na mauza2 yake kwan nimemmis sana.

Kan alisema ...

habari Dear/samahani kama nitakukwaza naju blog ni yako,lakini kuna kitu kimenishangaza mimi nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa hadithi na blog yako kwa ujumla, sasa ukawa unatuhadithia hadithi mbalimbali lakini kabla hadithi hizo hazijaisha, ukaacha, then umeamua kuanza upya hadithi hizo kwa ambao hawajazisoma, sijaelewa logic behind this, naomba unisaidie kunielewesha.

emu-three alisema ...

Tupo pamoja mpendwa, UPO JUU!

dj cany alisema ...

pa1 xana.. upo juu kama mawingu..!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom