Jumanne, Oktoba 08, 2013

KUWA MAKINI WEKA MBALI NA WATOTO

Kutokana na hali halisi ya UTANDAWAZI, ni wazi kabisa watoto wanajua kutumia  computer wakiwa na umri mdogo  jambo ambalo ni zuri kama watatumia vizuri kwa manufaa ya kujifunza yale yenye manufaa kwao lakini tatizo linakuja siku hizi kutokana na mitandao mbalimbali ya kijamii, kumekuwepo na picha mbalimbali za ajabu, ambazo zipo kwenye mitandao.

 Kwa kiasi kikubwa mzazi usipokuwa makini mtoto wako atakuwa ni mmoja kati ya wale wanaopenda kutizama picha za matusi. Kuna baadhi ya watu  huziweka picha hizi katika simu zao na haswa kwenye computer na wakati huohuo unakuta mtoto huwa anatumia hiyo computer  pale inapokuwa ipo nyumbani na kwa namna watoto walivyo watundu wanapenda kujifunza kila kitu basi anaweza kuziona zile picha na hapo utakuwa unampotosha mtoto.

Vilevile zipo DVD ama VCD za wakubwa ambazo kwa kiasi kikubwa kama utakuwa umeweka vibaya basi ni rahisi mtoto kuichukua na kuitizama huku akijifunza kile anachokiona. Ni muhimu kwa wazazi kuweka mbali na watoto picha ama video za matusi ambazo hazimjengi mtoto bali inasababisha Mmomonyoko wa maadili ambapo ni UGONJWA UNAO HATARISHA USTAWI WA NCHI. 


 Ni jukumu la kila mmoja kwa nafasi yake kuanzia viongozi wa dini, familia na hata ngazi mbalimbali za serikali kuhakikisha Tanzania yenye maadili inajengwa.  FUTA DELETE KABISA PICHA AMBAZO HAZINA MAADILI KWA WATOTO. WEKA MBALI NA WATOTO.



Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom