Ijumaa, Machi 14, 2014

KIPIRA CHA KUZUIA VVU KWA WANAWAKE CHAGUNDULIWA


Wakati bado kuna utata kuhusu tiba halisi ya ugonjwa wa Ukimwi duniani, wataalamu wamebuni kipira maalumu kinavyowekwa kwenye uke na kuzuia maambukizi ya  VVU. Mtafiti Patrick Kiser wa chuo Kikuu cha Evanston, nchini Marekani  amesema harakati za kupambana na ugonjwa  wa ukimwi zinafanyika kwa hali na mali ili kuwalinda wanawake wasipate maambukizi ya VVU. Anasema "Tatizo kubwa ni pale ambapo mwanamke anapata mwenza ambaye hataki kuvaa mipira ya kiume. Kwahiyo kipira hiki kitamsaidia mwanamke kujilinda na maambukizi.

 Kipira hicho kimetengenezwa kwa kuchanganywa na dawa aina mbili tofauti ambazo ni Tenovofir (ya kuzuia maambukizi ya VVU) Na dawa ya kuzuia ujauzito na maradhi mengine ya zinaa. Kipira kikishawekwa kinafanya kazi kama kawaida na huweza kutolewa kwa muda  baada ya tendo  na baadaye  kukirudisha wakati wa tendo. CHANZO MWANANCHI

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom