Alhamisi, Machi 13, 2014

MKE AUA MUME CHANZO MCHEPUKO NJE YA NDOA YAO

Mwanamke Etina Silumba mwenye umri wa miaka 44 mkazi wa kijiji cha Mpemba  wilayani Momba anashikiliwa na polisi mkoani Mbeya.Kamanda wa Polisi mkoani hapo. Ahmed Msangi  alisema mume aliyeuawa alitambulika kwa jina la  Mwisheck Mwashiuya (52) mkazi wa Mpemba wilayani Momba.Tukio hilo limetokea machi kumi ikiwa zimepita siku mbili tangu kuadhimishwa kwa kilele cha siku ya wanawake Duniani.
 Alisema mwanamke huyo alitenda unyama huo kwa mumewe majira ya saa tatu usiku katika kijiji cha Ipapa kata ya Ipunga wilayani Mbozi. Mwanamke huyo alimuua mumewe kwa kumkata kisogoni na kitu kinachosadikiwa kuwa ni panga kabla ya kumvunja shingo na mguu wa kushoto. Uchunguzi umebaini kuwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi na kuwa kabla ya tukio wanandoa hao walikuwa na ugomvi  wa kutuhumiana  kuchepuka nje ya ndoa. yao. Mwanamke huyo atafikishwa mahakamani baada ya taratibu kukamilishwa na kusisitiza kwa kuwataka wanajamii kutumia njia ya mazungumzo kusuluhisha migogoro baina yao badala ya kutumia mabavu.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom