Jumatatu, Machi 31, 2014

RIPOTI YA UMOJA WA MATAIFA IMEONYA "Mabadiliko ya tabia nchi duniani huenda yakaleta madhara makubwa zaidi na ambayo hayawezi kurekebishika"


Wanasayansi na maafisa wanaokutana nchini Japan wamesema ripoti hiyo imefanya uchunguzi wa kina kwa sasa kuhusu athari za mabadiliko ya tabia nchi duniani.
Wajumbe wa jopo la Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya hali ya hewa, wamesema ripoti hiyo inatoa ushahidi wa kutosha wa kiwango cha madhara hayo.
Mifumo asilia kwa sasa haufanyi kazi sawasawa, lakini ongezeko la madhara kwa binadamu ndilo jambo linalohofiwa zaidi.
Afya zetu, makaazi, chakula na usalama vyote viko katika hatari kutokana na kuongezeka kwa viwango vya joto, ripoti hiyo inasema.
Ripoti hiyo ilipitishwa baada ya majadiliano ya kina yaliyodumu kwa wiki moja mjini Yokohama. CHANZO BBC SWAHILI.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom