Jumanne, Aprili 22, 2014

MASIKINI AMINA


Amina ni msichana mdogo mwenye umri wa miaka 17, ilitokea akiwa kidato cha pili akapata ujauzito na kwa wakati huo alikuwa na umri wa miaka 15, kutokana na hali hiyo wazazi walihuzunika sana, na baba yake alichukia sna kumtaka aondoke nyumbani na kwenda kuishi na mwanamume aliyempa ujauzito, lakini mwanaume aliyekuwa amempa ujauzito pia alikuwa ni mwanafunzi, hivyo  Mama yake na Amina alijaribu kumbembeleza mzazi mwenzake na baadaye Amina alibaki pale nyumbani huku akiwa anaishi katika mazingira magumu, Baada ya miezi tisa alijifungua kwa shida kutokana na umri wake kuwa mdogo, Baada ya muda alitamani kuendelea na masomo lakini alipowaeleza wazazi wake walikataa na kumtaka aolewe. 

"Wazazi wangu walisema huo ndiyo mwisho wa elimu yangu kwani  kilichobaki natakiwa niolewe kuhusu suala kusoma nisahau kabisa, ijapokuwa niliwaomba wanisamehe  kwani sasa siwezi kurudia kosa na nitasoma kwa bidii walikataa na baba alisema hawezi kupoteza pesa juu yangu" Alisema Amina ambaye ana mtoto mdogo mwenye umri wa mwaka mmoja. Hizi ni changamoto ambazo wanapata  wanafunzi wanaopata mimba za utotoni huku. Suala la wanafunzi wajawazito wakijifungua kurudi shule limekuwa likizungumziwa mara kwa mara lakini bado baadhi ya wazazi hawakubaliani na suala hilo.


Chama cha wanahabari wanawake Tanzania (Tamwa) na wadau mbalimbali wa haki za mtoto na wanawake wamekuwa wakifanya kampeni mbalimbali ili kukabiliana na tatizo la  ndoa na mimba za utotoni.Limekuwa ni tatizo sugu katika maeneo mbalimbali ya nchi hii. Watoto wengi wanaopata mimba maranyingi ni wanafunzi wa shule za msingi au sekondari Matokeo ya watoto hawa kupachikwa mimba huwasababishia kuacha masomo na baadhi yao kwenda kuolewa. Wengi wanajuta baada ya kuwa wamepata mimba, lakini fursa ya kuendelea na masomo huwa imewaponyoka. Vilevile baadhi ya wazazi wanadaiwa kushinikiza mabinti waolewe katika umri mdogo kwa tamaa ya kupata mahari. Utafiti uliofanywa na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania mwaka jana umeonyesha kuwa matukio ya aina hiyo ni mengi katika maeneo ya vijijini na yamekuwa yakifanyika kwa usiri

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom