Jumatano, Aprili 16, 2014

Uamuzi huu ni wa kihistoria India "Watu waliobadilisha jinsia yao kutambulika kama watu wa kawaida katika jamii"

Mahakama ya juu zaidi nchini India imetoa uamuzi wa kihistoria unaotambua watu waliobadilisha jinsia yao kama watu wa kawaida katika jamii. Kawaida kuna jinsia mbili, mke au mume lakini mahakama hiyo imesema kuwa watu wanaoamua kubadilisha jinsia yao kuambatana na hisia zao pia ni lazima watambuliwe na jamii. Mfano wa watu kama hao ni mtu anayezaliwa kama mwanamke lakini anahisi kisaikolojia kuwa yeye ni mwanaume na hivyo hubadilisha  jinsia yake na kuwa mwanamume kwa kufanyiwa upasuaji.

 Uamuzi huu wa mahakama bila shaka ni wa kihistoria. "Ni haki ya kila binadamu kuchagua jinsia wanayoitaka" Alisema jaji katika uamuzi huo ambao unawapa watu haohaki ya kujitambulisha kama wanaume au wanawake.Mahakama pia imeamuru serikali kuwapa watu hao nafasi za kazi na elimu kama jamii ya watu waliotengwa na kuwapa huduma muhimu watu hao wanaochagua kujitambulisha watakavyo.

 Takwimu zinaonyesha kuwa watu milioni mbili nchini India wamebadilisha jinsia yao. "Watu hawa ni raia wa India na lazima waheshimiwe na kupewa nafasi ya kuanawiri maishani" Alisema jaji katika uamuzi wake. "Lengo la katiba ni kuhakikisha kila mtu wa India anapewa nafasi ya kuishi vyema na kujiendeleza maishani licha ya jinsia, na jamii anakotoka.BBC.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom