Jumatatu, Aprili 14, 2014

Ujumbe wa Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Innocent Mungi kwa wanafunzi. "Mkiachana na matumizi mabaya ya mitandao mtapata ajira"

Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Innocent Mungi. Amewatahadharisha wanafunzi wa chuo cha Uhasibu Arusha kuepuka lugha potofu na uwekaji wa picha zisizo na maadili kwenye mitandao ili kukidhi haja kwenye soko la ajira. Ilikuwa ni siku  ya wanafunzi wa chuo hicho kuongea na waajiri na wanafunzi iliyoandaliwa kwa lengo la kufahamu hali halisi kwenye soko la ajira pindi watakapomaliza masomo yao.
 Alisema Teknolojia imekuwa kwasasa kila mwajiri akitaka kuajiri mtu au mtaalamu yeyote anaangalia kwenye mtandao kama muhusika hana kashfa na ni mwadilifu, hivyo ni vyema wakajiepusha na vitendo vya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamiii ili wasije kulia baadaye "Mkiachana na matumizi mabaya  ya mitandao mtapata tu ajira, ila shida vijana wengi sana mnajikuta katika mkumbo huowa kutumia vibaya mitandao badala ya kuitumia kujifunza na matokeoyake kwasasa mbaya unajikuta ukikosa kazi.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom