Jumamosi, Aprili 26, 2014

WANAVYOSEMA BAADHI YA VIONGOZI KUHUSU SIKU YA LEO,MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO.

Miaka 50 ya muungano huu kuna mambo mengi mazuri yamefanyika ambayo yanaufanya uwe wa mfano duniani. Muungano wa Tanganyika  na Zanzibar ni matokeo ya kupata jina Tanzania.Tanzania ilipatikana kwa juhudi za waasisi wa nchi hizi mbili Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Abed Karume waliosaidia kuujenga muungano huu. Tarehe 26/April1964 tulipata taifa linaloitwa TANZANIA na kuwekwa kwenye ramani ya Dunia kama Tanzania. Miongoni mwa mambo yaliyofanyika ni kudumisha amani na utulivu, kuanzishwa na kukamilishwa kwa miradi ya maendeleo pia kuimarika kwa uhusiano baina ya wananchi wa bara na visiwani.

"Wapo wenzetu barani Africa walijaribu lakini hawakufanikiwa kama sisi, kwani muungano wao ulidumu muda mfupi na kusambaratika, wapo waliokaa miaka miwili, miezi nawapo ambao wameanza majadiliano mpaka leo hawajamaliza" Amesema Rais Jakaya Kikwete Muungano wetu ni mfano wa Afrika.
"Tanzania ni Lulu ya kipekee kabisa katika historia ya Afrika, nchi nyingine zote ni za kurithi kutoka ukoloni, Tanzania ni ya kuundwa na sisi wenyewe  kwa hiari yetu wenyewe baada ya kukomboa sehemu zake kutoka ukoloni, mafanikio yaliyopatikana Tanzania yanaonyesha kuwa pia shirikisho la Africa Mashariki linaweza na nchi za bara la Africa kuungana na kuwa nchi moja inawezekana" Alisema Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

"Katika miaka hii 50 ya muungano ni kweli kuna kero za muungano, lakini nyingi zimepatiwa ufumbuzi tofauti na mwanzo na nina imani zitaendelea kupungua, nawaomba watanzania wote, viongozi wa vyama vya siasa wasomi na wananchi tujitahidi sana kuenzi muungano huu kwani una faida kubwa hakuna kitu ambacho hakina matatizo hata madogo hivyo ni vyema kukaa na kutatua matatizo yetu bila kudhoofisha Muungano wetu" Amesema Paul Kimiti miongoni mwa viongozi wastaafu wa serikali ambaye amefanya kazi na muasisi wa Muungano hayati Baba wa Taifa.



"Nakerwa zaidi na Zanzibar kuwa na katiba yao, wakati katiba ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inasema Zanzibar ni sehemu ya nchi yake pia.Wakati wa sherehe za muungano  Rais wa Zanzibar ndiye anaonekana mwenye nguvu kitu ambacho siyo sahihi Rais wa Tanzania ndiye apewe hadhi kubwa 

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom