Ijumaa, Mei 09, 2014

Wasemavyo wataalamu "Tabia na mienendo ya watu kimaisha ni sababu ya matatizo kwao"

Afya ya mtu yeyote inategemea sana namna anavyokula anavyoishi na kujiweka katika mazingira yanayomzunguka ili kujikinga na maradhi "Wataalamu wa afya wa jamii wanasema kuwa takribani asilimia 53 ya magonjwa ya binadamu husababishwa na mtindo wa maisha usiofaa kwa mfano ulafi,ulevi,kubweteka bila kufanya kazi ngumu, kutofanya mazoezi pamoja na ngono zembe" Wanasema matibabu mengine hayaitaji tiba za dawa kali au kuchomwa sindano, mtindo wako wa maisha waweza kuwa bora kabisa, unaambiwa kupumzika kula mlo kamili na kupima afya vyaweza kuwa tiba. Daktari mmoja aliwahi kusema "Mbogamboga na matunda ni dawa nzuri zaidi kuliko dawa za Hospitali".

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom