Jumatatu, Juni 16, 2014

”KUPATA ELIMU BORA NA ISIYO NA VIKWAZO NI HAKI YA KILA MTOTO.”



kila mwaka June 16 Umoja wa Afrika sambamba na washirika wake husherekea siku ya mtoto wa Afrika- ikiwa ni kumbukumbu ya mwaka 1976 ambapo waandamanaji wanafunzi wa shule za Soweto Afrika ya Kusini waliandamana kupinga elimu iliyokuwa inatolewa kwa manufaa ya utawala wa kibaguzi wa makaburu. Maandamano hayo yalipokelewa na mikono usio na huruma na masikio yasiyo sikivu ya utawala wa kibaguzi na kusababisha vifo vya mamia ya wanafunzi 

Kwa mwaka huu yaani 2014 Umoja wa Afrika umetaja lengo Kuu la Siku hii ni kuzitaka serikali zote barani humu kutekeleza majukumu yake ya kuhakikisha watoto wanapata haki ya kupata elimu bora kulingana na mikataba mbalimbali juu ya haki za mtoto ya kimataifa inayosema. Pakiwa na kauli mbiu,”KUPATA ELIMU BORA NA ISIYO NA VIKWAZO NI HAKI YA KILA MTOTO.” Sio kusema kuwa haki zingine za mtoto zinazikwa katika kaburi la sahau bali Umoja wa Afrika umeziambatanisha haki zingine katika malengo mahususi kwa mwaka huu. Kulingana na ripoti ya hali ya mtoto wa Afrika iliyotolewa miaka minne iliyopita ilibainisha kuwa elimu katika mataifa mengi ya bara hili imezingwa na matatizo mengi yakiwamo wanafunzi wengi wanaomaliza shule kutokuwa na uwezo wa kutosha kulingana na elimu yao, huku wanafunzi wengi wakiacha masomo kwa sababu mbalimbali zikiwamo mimba, na kukosekana kwa umakini wa kutiliwa mkazo kwa elimu ya awali ambayo inamjenga mtoto katika kupata elimu ya msingi.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom