Jumamosi, Julai 19, 2014

CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE TANZANIA (TAWLA) CHAZINDUA HUDUMA YA SIMU BILA MALIPO "TOLL FREE LINE"


Kutokana na asilimia kubwa ya wanawake nchini kushindwa kufikiwa ma huduma za kisheria bure na sababu ikiwa ni hali duni ya kifedha  pamoja na mawasiliano baina ya vyombo husika vinavyotetea haki ya wanawake. Akizungumza katika uzinduzi wa  huduma ya simu bila malipo "toll free line"  Mwenyekiti  wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) Aisha Bade amesema "Jambo la kutofikiwa kwa upatikanaji wa haki linaweza kusemwa, kwani ni mojawapo ya mambo makuu yanayochangia unyanyasaji kwa wanawake na bila kupata haki zao za msingi". 

Amesema Kutokana na hali hiyo chama hicho kimeamua kuzindua huduma ya simu bila malipo ambayo walengwa wa huduma hiyo ni wanawake walio katika mazingira magumu. Ameongeza kuwa huduma hiyo pia itatoa fursa y kutoa ushauri  wa kisheria kutoa mwongozo juu ya kujiwakilisha katika mashauri mbalimbali yaliyombele ya vyombo vya maamuzi pamoja na kutoa maelekezo na rufaa kwa mashirika mengine ikiwemo ustawi wa jamii au chombo husika kulingana na asili ya kesi. 

 Amesema mteja akipiga simu atasikilizwa na mawakili au maofisa sheria waliopata mafunzo maalumu kwa huduma hiyo na kuchukua taarifa zao ambapo namba za huduma hizo ni pamoja na 0800751010 na 08800110017.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom