Alhamisi, Julai 24, 2014

UJUMBE WA LEO KUTOKA KWA WAZIRI MKUU MSTAAFU SUMAYE "Wizi Wa Kura utatuponza"

Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, amesema wizi wa kura na uchakachuaji wa matokeo ya chaguzi, ni miongoni mwa vitu vinavyosababisha vurugu na kufifisha amani kwa nchi na watu wake.“Wakati mwingine hali hii hutokea kwa upande mmoja kukataa kushindwa hata kama wameshindwa kwa halali. Jambo hili la kisiasa limeleta fujo nyingi hasa katika nchi nyingi za Kiafrika na kusababisha umwagaji wa damu,” 


“Ni lazima shughuli zetu za siasa zifuate sheria na taratibu zilizowekwa kwa uwazi bila kutiliwa shaka na upande wowote. Haki ni lazima isimamiwe kikamilifu nyakati zote za kampeni hadi upigaji wa kura, kuhesabu kura na hata kutangaza matokeo,” alisema. Pia chuki zinazoelekezwa kwenye imani za kidini zinapaswa kukemewa kutokana kuwa na madhara yanayoiathiri jamii nzima.

Amesema hivi sasa kuna chokochoko zenye sura ya imani zinazochangia kufifisha upendo na uzalendo, hivyo kuathiri umoja uliopo. “Tukiwa wamoja hili halina nafasi kwa sababu hakuna dini inayofundisha chuki kwa binadamu mwenzake,” Viongozi wa dini wanapaswa kuwasimamia waumini wao, ili nchi isije ikakumbwa na balaa la vurugu za kidini, jambo ambalo ni la hatari na lisilopaswa kutokea. 


 kushamiri kwa tofauti kubwa ya kipato baina ya makundi tofauti, hasa kati ya matajiri wachache na wenye madaraka kwa upande mmoja na maskini walio wengi kwa upande wa pili. Alisema tofauti hizo zinasababishwa na mfumo mbaya wa uchumi na ubinafsi uliokithiri ama usiojali binadamu wengine. 



“Hali hii ni ya hatari kwa amani na utulivu kwa sababu walio wengi hawatavumilia kuwaona wachache wakiishi katika anasa za kutisha wakati wao hawamudu hata mahitaji ya lazima kama vile chakula, matibabu na maji,” alisema.Alisema hali kama hiyo imesababisha vurugu katika nchi nyingi na kuathiri amani na utulivu na kwamba hata hapa nchini, kuna tofauti kubwa ya kipato kwa makundi hayo hivyo inahitajika kudhibitiwa kwa haraka. 

kutokana na hali hiyo, ipo haja ya kuwekeza na kutekeleza mipango inayochochea uzalendo wa kuipenda nchi na watu wake. Kukosekana kwa umoja ni miongoni mwa sababu zilizofifisha maendeleo katika nchi nyingi za Bara la Afrika. 

Aliongeza: “Siku hizi hutokezea hata katika chaguzi za nafasi za uongozi makanisani watu kujitenga na viongozi waliochaguliwa eti kwa sababu tu huyo aliyechaguliwa hakuwa chaguo lake, hali ambayo huwafanya viongozi kuongoza kwa shida sana.”Aliyasema hayo wakati akihutubia mkutano mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Kati, uliofanyika jana jijini Arusha. Ujumbe wake ulijikita katika uwapo wa umoja, amani na utulivu.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom