Jumatatu, Oktoba 27, 2014

JIFUNZE JAMBO KUPITIA SIMULIZI HII FUPI.


Ulikuwa ni usiku mtu mmoja akiwa anajiandaa kulala rafiki yake akamwambia ni vyema kumshukuru Mungu kabla ya kulala, Mtu huyo akasema "Najisikia kuchoka sana leo siwezi kusali, nitasali kesho wewe niombee katika sala zako, basi akapanda kitandani na kulala wakati usingizi ukiwa unampitia taratibu simu yake ya mkononi iliita alipokea na aliyempigia alimtaka ajiandae anampitia waende club usiku huo, Mtu huyo bila kupoteza muda alinyanyuka kitandani na kuanza kujiandaa haraka, mwenzake aliyekuwa anasali alimtizama na kusema "Wewe si umesema umechoka, mbona unajiandaa kwenda club".

Mtu huyo alikuwa anaitwa Mkelele, aliendelea kujiandaa, bila ya kumsikiliza mwenzake, baada ya muda aliondoka kwenda club, huku akimuacha rafiki yake akisikitika sana, alifika club na kujichanganya na marafiki zake wengine ambapo walicheza na kunywa sana pombe, ilipofika majira ya saa kumi za usiku walianza safari ya kurudi nyumbani, wakiwa njiani walikutana na majambazi, hivyo walivamiwa na kunyang'anywa kila kitu. 


Wale majambazi walikuwa na silaha na kwa namna walivyokuwa wamelewa walishindwa kupambana nao, hali ya Mkelele ilikuwa mbaya sana kwani alipoteza fahamu alipozinduka alijikuta yupo hospitalini, na aliyekuwa amesimama pembeni yake alikuwa ni yule rafiki yake ambaye wanaishi pamoja alimtizama na kusema, "Najuta sana, kwani yote haya yasingenikuta kama ningekusikiliza, nisamehe rafiki yangu kwani shetani alinipitia".

Rafiki yake alitabasamu na kusema "Mungu ni kila kitu katika maisha yetu,kwani hata kama umechoka kwa kiasi gani, angalau utaje neno moja tu la kumshukuru kwani bila yeye hakuna linalowezekana, na pia ulivyoondoka nilikuombea sana kwa Mungu akusamehe kwani ulikuwa hujui utendalo , Mshukuru sana Mungu kwani amekupa nafasi nyingine" Basi tangu siku hiyo Mkelele alimshirikisha Mungu katika kila jambo analofanya, na maisha yake yanaendelea vizuri bila matatizo yoyote.nimatumaini yangu kupitia simulizi hii fupi naimani kuna kitu ambacho utakuwa umejifunza. NA ADELA DALLY KAVISHE

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom