Jumatatu, Machi 02, 2015

UJUMBE WA LEO NA DINA MARIOS "kIla wakati nikimuangalia mwanangu najiuliza nitaweza kuwepo kumlinda kila mahali"

Dunia hii yenye vurugu na watu kuwa na imani ndogo unyama mwingi mwanangu ataishije?
Je nitaishi miaka mingi kumuona akikua na mimi kutimiza jukumu alilonipa Mungu la kuwa malaika wake hapa duniani?Mama yangu aliniacha mdogo sana nimekuwa kwa kukuru kakara nyingi,shida raha na karaha mbali mbali.Vyote vimenifanya kuwa imara hata lije jaribu gani nikikumbuka nilipotoka na nilivyoshinda hakuna jipyaa zaidi kwani nimeshakomaa.

Najiuliza je na yeye atakuwa imara?hatatetereka na kupoteza uelekeo?
Je nitafanikiwa kumlea ipasavyo na akafata njia zimfaazo?Atakuwa mwema,mcha Mungu,mwenye upendo,mkarimu na mwenye busara.Hatakuwa katili na muonevu kwa binadamu wengine. Kila wakati namtazama na kumuombea naweza kuamka hata usiku sana namtazama na kumuombea.
 
Uoga nilionao ni kila mama anao?naomba Ulinzi wa Mungu uwe nae kila wakati.Hata nikiwa sipo nyumani naomba nirudi na nimkute salama.Tusichoke kuomba kwa ajili ya watoto wetu hasa kina mama.Ndio maana katika familia mama akifa watoto hubaki wakitaabika.Mama akiwa hamjui Mungu watoto huenda bila dira.Mama akiwa legelege watoto nao huwa hawana mhimili imara.Mimi ni mama mpya lakini tayari ni mama sihitaji kuwa na watoto sita kuelewa hii.

Kila wakati tuombee watoto wetu na kuwakabidhi chini ya ulinzi wa Mungu.

Maoni 2 :

Bila jina alisema ...

Amenena maneno mazuri sana . Ila Mungu ndo milinz zaidi kwani yy alilelewa bila mama na leo ni mdada mwenye busara na anajitambua .Hana skendo mjini na anajitambua . Wako wazazi wanawake wtt ktk sifa zote na ikapita sheteni nawadanganya wanapotea. MUNGU TUBSRIKI WAZAZI WOTE TUWALEE WATOTO NA WTOTO VWATUTII
MUNGU WEWE NDO MLINZI ONA HATA WATOTO ALBINO WANACHUKULIWA MIKONONI MWA MAMA ZAO KISA PESA

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom