Katika mahusiano ili uone raha yake lazima muwe mmekubalina na mnapendana,,mfano katika picha hii inaonyesha wapenzi hao wakiwa wamekubalina na mahaba mazito yakiwa ndani yao.,Jamani mapenzi hayalazimishwi..
Kuna tukio limetokea huko mkoni Manyara ambapo Jeshi la polisi linamshikilia mwanamume mkulima wa Ibwaga Wilaya ya Kongwa kwa tuhuma ya kumuua mwanamke katika mazingira ya kutatanisha.. Siku ya tukio mtuhumiwa alimtaka kimapenzi kwa nguvu Marehemu Pili Loringa(28) mkazi wa Mnasi mkoani Dodoma,lakini marehemu alikataa kitendo kilichomuudhi mtuhumiwa na kuamua kumuua kwa hasira ya kunyimwa mapenzi..
Akizungumza na gazeti Mwananchi Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara amesema marehemu alikutana na mtuhumiwa njiani wakati akitoka dukani ndipo alipomtaka kimapenzi, hata hivyo wakati akiuawa alipiga kelele ya kuomba msaada ndipo wananchi walipoenda sehemu ya tukio na kumkuta tayari alishauawa na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa..jamaa linashikiliwa ma polisi huku upelelezi ukiendelea
Wakazi wa eneo hilo wamelaani kitendo hicho na kusema mwanamke huyo amekufa kishujaa,,kwani kwa kukataa uasherati alikuwa akitimiza maagizo ya Mwenyezi Mungu na kwamaba alikuwa akitekeleza kampeni za wanawake hatudanganyiki..
|
Maoni 4 :
Daaah! hii kitu inawezekana sana kutokea katika jamii zetu, haswa katika masuala ya mapenzi as u said, na tabia hii ipo sana kwa wote men/women, utakuta mtu anakataliwa kimapenzi, et coz of umaarufu wake au pesa zake alizokuwanazo, anaamuwa kufanya mamboz kama haya ya kuuwana, yaani anaona bora kumuuwa mwenziwe ili atunze heshima yake katika jamii, watu wasimzarau, au ndio anaona anamtia adabu mwenziwe kwa njia ya sumu au yoyote ile, hajuwi kwamba ipo siku na yeye atakufa, kama umekataliwa jamani sema na moyo wako, au angalia mapungufu yako, sio uanze kutumia uwezo wako na kumdhurumu mwenzio uhai wake!! Thanks Adela..
Duuuh,mambo haya yanatokea mara nyingi tuu katika jamii zetu...
'Mimi sidanganyikiii' huo ni usemi mzuri, na kutokudanganyika huko, kusiishie tu kukataa, lakini pia mtu asikubali kupelekwa vichochoroni, au vichakani, kwani inaonyesha kuwa ulikuwa unapenda lakini kikaja kitu fulani kikakutaza, au ikawa hailipi!
Kataa kwelikweli, kwani ni haki yako, na mlazimishaji ana hatia kubwa sana, sio hapa tu lakini hata kwa mola ataipata fresh
@Hashir asante sana@Edna asante pia wangu@Emu three tuko pamoja...huo ni ubakaji na ukatili mkubwa.inauma sana.
Chapisha Maoni