Jumanne, Novemba 16, 2010

Christina Milian Kimwana asiyetaka tena kuolewa,,ndoa yake na the dream ilidumu kwa muda wa chini ya miezi minne.

Muimbaji na muigizaji christina Milian pichani anapanga kubaki single kwa muda mrefu baada ya kutengana na mumewe The Dream amesema Nitabaki kuwa single kwa miaka mingi aliliambia jarida la people sina mwanaume maishani mwangu napenda kuwa peke yangu nimeshahama kutoka mahusiano hadi mahusiano na hii ni mara ya kwanza kujisikia huru na amani zaidi nikiwa peke yangu.Muimbaji huyu ambaye alifanya vizuri na kibao cha Deep it Low amesema kwa sasa anajisikia huru na anapenda kuwa single.

Christina Milan pichani akiwa na aliyekuwa mume wake The dream.

The dream na Christina Milian walipofunga ndoa mjini Las Vegas September 2009 na kuzaa naye mtoto wa miezi nane anyeitwa Violet.The dream anadaiwa kusaini fomu za talaka siku tisa kabla Christina hajajifungua na alidai kwamba ndoa yao imevunjwa magazetini.Tangazo la talaka baina yao lilifuatia  picha za utata zilizomuonyesha The Dream akijiachia ufukweni na mwanamke mwingine

Pichani The dream akiwa ufukweni na kimwana aliyeleta mtafaruku katika ndoa yao.

Christina Milian na binti yake Violet, Hivi karibuni Christina na The dream waliripotiwa kufikia muafaka nje ya mahakama kuhusu kesi yao ya talaka,ambapo kimwana huyo amefarijishwa na hali hiyo na amesema ni bora kwani ni manufaa kwa binti yao ambaye amesema anafikiria kufanya kila kitu kwa ajili ya mtoto wake na anataka maisha bora kwa ajili yake huku akimsifia na kusema ni binti mwenye furaha na ni mtoto mrembo sana.

Jamani walikuwa wanapendeza sana kuwa pamoja lakini ndio hivyo wamedumu kwa muda mfupi sana katika ndoa na kwa sasa kila mmoja ameshazoea maisha ya kuwa peke yake. Jamani mapenzi hayatabiriki ni muhimu kuwa makini  kwani inawezekana wengine wakasema mapenzi ya watu maarufu hayadumu lakini wapo waliodumu muhimu kujitambua na kuwa na uhakika na maisha unayoyataka. Chiristina sasa hataki tena kuolewa sijui labda baadae atabadilisha mawazo mtoto akishakuwa mkubwa...

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom