Hali ya migogoro katika mahusiano ni jambo ambalo linatokea mara kwa mara, lakini inapotokea hali kama hiyo ni vizuri kujua nini cha kufanya kwa kukaa pamoja na kuzungumza ili kupata ufumbuzi wa tatizo.Kuna baadhi ya watu katika mahusiano akigombana na mpenzi wake basi atasimulia kwa kila mtu hususani mashoga zake nk kitu ambacho sio kizuri kwani inasababisha watu kuwafahamu undani wenu zaidi. Mwingine kutokana na ugomvi ndani ya nyumba basi anaanza kutoa siri zote za ndani ya nyumba akiwa amekaa na marafiki zake huku akimkashifu mwenza wake sasa ikitokea mmepatana sijui utarudi kumsifia tena kiukweli sio tabia nzuri hata kidogo..BE CARE TUNZA SIRI ZA NYUMBA YAKO |
Maoni 1 :
Saa nyingine inawezakuwa ni MSAADA kuongea na MTU mwingine matatizo yako kwa kuwa mtu mwingine anaweza kuliona tatizo lilipo kirahisi zaidi hasa kama wahusika kwenye PENZI mko ndani ya migongano na HASIRA zimetawala.
Unajua tena HASIRA hupofua baadhi ya busara ambazo huweza kuwa ndizo zenye jibu ya TATIZO.
Cha muhimu ni kuwa ujue ni nani wa kumuamini na siri yako katika udhaifu. Na kumbuka tu kuwa wakati unaongelea tatizo lako isiwe tu lengo ni kumdhalilisha mwenzio na sio kweli kutafuta kuelewa kiini cha tatizo.
Chapisha Maoni