Pages

Jumanne, Novemba 09, 2010

Mama adaiwa kutaka kumuuza mwanaye kwa mganga ili apate sh. milioni 60 na kulipa deni analodaiwa...

Inapendeza mama kama huyu akiwa na mtoto wake na kumlea katika mazingira yoyote ikiwa ni katika hali ya shida au raha,lakini kutokana na hali ya maisha kuwa ngumu baadhi ya watu hukata tamaa ya maisha na kujikuta wanafanya mambo ambayo sio sahihi kama matukio ya kuua au kujiua nk..

Huko Nchini Uganda Jeshi la polisi linamshikilia mwanamke raia wa nchi hiyo kwa tuhuma za kutaka kumtoa kafara mwanaye ili apate fedha za kulipa deni lililokuwa linamkabili. Habari kutoka Kampala zimeeleza gazeti la Alasiri kuwa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 20, alikamatwa jana akiwa katika harakati za kutaka kumuuza mwanaye kwa Mganga wa Kienyeji ili aweze kulipa deni la shilingi 210,000 alizokuwa akidaiwa kwa bahati mbaya ama nzuri akajikuta akiangukia mikononi mwa polisi.

 Baada ya kuwasiliana kimakosa na mganga mwingine ambaye alimkabidhi mikononi mwa Polisi.Baada ya kukamatwa na polisi mwanamke huyo alielezea jinsi hali ilivyo nyumbani kwake na nia ikiwa ni kupata fedha ili arejee shuleni,kulipa deni, kununua ardhi na kujenga nyumba hivyo kutaka kumtoa kafara mwanaye mwenye umri wa miezi 11 kwa mganga wa kienyeji kwa kitita cha shilingi milioni 60,imeelezwa kuwa hata hivyo mganga huyo alikataa kufanya biashara hiyo na kisha kumchomea kwa polisi akitoa ushahidi mganga huyo amesema aliamua kufanya hivyo ili kujisafisha jina lake kutokana na baadhi ya watu kumshutumu mara kwa mara kwa kutoa kafara watoto.sasa jamani kweli mtu yupo tayari kumtoa kafara mtoto wake ili afanikiwe duuuh inawezekana wapo wengi sana wanaofanya mambo hayo ya kutoa kafara ili kufanikiwa.


Maoni 3 :

  1. Duuuh, hii kali , duniani kuna mambo!

    JibuFuta
  2. Jamani maisha haya, kwa kweli inasikitisha sana na inaumiza roho

    JibuFuta
  3. Jamani dunia imeisha, taama gani hizo!!!!!!!! Mungu amsamehe kwa sababu hajui alitendalo

    JibuFuta

Unakaribishwa kutoa maoni yako.