Jumanne, Novemba 02, 2010

Mume wangu anataka nizae na rafiki yake kwasababu yeye hana uwezo wa kunipa ujauzito.




Mtoto huongeza furaha katika familia,,lakini inatokea wengine wanapata watoto lakini wengine wanatafuta watoto ikiwa ni kutokana na matatizo mbalimbali,,kuna mama mmoja kutoka Arusha anaomba ushauri jamani..

Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 33 nimeolewa nina takribani kama miaka kumi na miwili  tatizo ni kwamba sijafanikiwa kupata mtoto hadi hivi sasa,nilimshauri mume wangu tuende hospitali ili kujua nini tatizo, baada ya kwenda hospitali imegundulika kuwa mume wangu ndio mwenye matatizo sasa cha kushangaza ananiambia nizae na rafiki yake ili  tupate mtoto na iwe ni siri yetu kiukweli mimi hiki kitu kinaniumiza sana kichwa ni kweli mume wangu hana uwezo wa kupata mtoto lakini mimi ananichanganya na hiyo kauli yake ya kutaka mimi  nizae na rafiki yake tena kila siku ananikumbusha na ameshamuambia na rafiki yake amekubali sijui nifanyeje na mume wangu nampenda sana.

Maoni 4 :

Yasinta Ngonyani alisema ...

Nina wasiwasi kama huyo mume anampenda kweli mke wake kwa dhati mpaka amkabadhi kwa rafiki yake. Na mtoto atakuwa wa nani? mmmhhh kweli watakuwa mke na mume tena? nawaza tu kwa sauti.....

emu-three alisema ...

Huo ni mtihani,na mtihani kama huo utatuzi wake ni kukubali halihalisi mliyo nayo. Na cha muhimu ni upendo, kwani watoto ni kudra ya mungu, je una uhakika gani kuwa huko atakapotembea atapata mtoto? Na kwa hali hiyo upendo utakuwepo kweli, huoni kuwa ni kujizalilisha!
Ukumbuke kuwa dunia hii haina siri, ipo siku huyu mtoto atatonywa au litatokea jambo ambalo litamfanya agundue kuwa baba yake wa kumzaa sio huyo wa kumlea, na baba yake atakuwepo unafikiri nini kitakachofuata!
Ni kweli watoto ni furaha katika familia, lakini kuwapata sio kwa njia hiyo! Kama mnahitaji mtoto wa kulea wapo wengi!
Mhhh, hapo najua kuna watasema kama ingekuwa tatizo ni kwa mke, mume angeoa mke mwingine, lakini sasa tatizzo ni kwa mume, mke yupo safi! Mtihani!

ADELA KAVISHE alisema ...

@Yasinta umeonaeeh utata huu ni vigumu sana@Emu three tuko pamoja wangu nakukubali

Bila jina alisema ...

Bora waka asili "adopt" mtoto kuliko hiyo hatari anayotaka kukutia. Wote watamchukulia mtoto wa kwao kuliko kuzaa na mtu mwingine. Kwasasa huyo rafiki anakubali tu lakini mtoto mtamu acha, akikua huyo atawageuzia kibao anamtaka mwanae mtafanyaje?
Kuna hospitali kampala zinafanya IVF na watu wanapata watoto vizuri tu ingawaje ni ghali.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom