![]() |
INAPENDEZA KUWA NA FAMILIA BABA, MAMA NA WATOTO WOTE KWA PAMOJA WANAJUKUMU LA KUTUNZA FAMILIA YAO BILA KUTETEREKA.JITAHIDI KUJENGA AMANI NA UPENDO KATIKA NYUMBA YAKO. |
![]() |
INAPENDEZA KUWA NA FAMILIA BABA, MAMA NA WATOTO WOTE KWA PAMOJA WANAJUKUMU LA KUTUNZA FAMILIA YAO BILA KUTETEREKA.JITAHIDI KUJENGA AMANI NA UPENDO KATIKA NYUMBA YAKO. |
Maoni 3 :
Kwanini ukwepe majukumu, hii inaonyesha udhaifu wa kutafakari, kwani matunda ya mapenzi ni pamoja na kupata watoto.
Sasa watoto wanapokuwepo, wanahitaji huduma na upendo wa pande zote mbili. Na tunasahau kuwa upendoo wa dhati hunazia kwa baba na mama. Hawa waili wakipendana na kusaidiana hujenga mzizi au msingi kwa kizazii chao, na ikiwa kinyume chake, utaona matokeo yake.
Sasa hivi vizazi vingi vinakuwa katika mmzazi mmoja, baba hakuna, au mama hakuna, ...unategemea nini hawa watoto wajifunze, wanakosa `upendoo ule wa asili ' wa baba na mama.
Na zaidi ya hayo,familia nyingi zinatelekeza majukumu hayo kwa wafanyakazi wa nyumbani,...
Oh, ni hayo yo mendwa Adela
Ila tukumbuke tu kuna watu wanogewao na PENZI na kusahau kuwa ndoa ni kitu tofauti na mapenzi ya High School au hata vyuoni.
Na kama wasemavyo watu fulani kuwa LOVE is blind- basi utakuta jamaa wamependana na kufanya maamuzi ya ndoa na kustukia tu baada ya kufunga ndoa kuwa kwanza hawashabihiani. Kuna wengi ambao ni mpaka baada ya ndoa ndio huanza kuishi pamoja na kuanza kustukia mpenzi yule mliyekuwa mnakutana tu kwa mihadi labda sio yule yule ukiishi naye kwa kuwa kwa kuishi na mtu ndio unaweza kustukia yake mengine ya kukerayo.
Sasa hapo ukiingizia na watoto na labda mpaka ndugu , mashoga nk,....
...unaweza kukuta mtu yuleyule hana ladha tena uzikumbukazo zilizo kufanya ujifie mwanzo..
Ukihitimisha na jinsi BINADAMU wanavyopenda kurahisisha mambo, waweza kuta kuna watu kukimbia nyumba ndio tatuzi kwa kuwa nyumba ndogo inaweza kuwa haiumizi kichwa na matatizo yaleyale ya nyumba kubwa hasa ukizingatia labda ndio ikumbushayo mtu mapenzi yake ya HIGH School.
Ndio maana naamini ni hatari kujiingiza kichwakichwa kwenye ndoa na kuzaa watoto hasa kama mpenzi mwenyewe mnajuana kwa juujuu na wala hujawahi hata kumuuguza akiumwa magonjwa fulani ya kifichoficho kama vile kuharisha vile.
Ndio,....
....kwa wengi ``LOVE IS BLIND´´ kitu kiwezacho kuwa ndio sababu ya watu kuingia kichwakichwa kwenye ndoa. Na love ni BLIND -kitu kiwezacho kuwa kinafanya mtu huyohuyo aanze kunogewa na mesenja kazini na kutotaka kurudi nyumbani kwa kuwa MZAZI mwenza siku hizi ni fulu kunuka kikwapa kujipenda hajipendi tena kwa kuwa YUKO KWENYE ndoa tayari.
Nawaza tu kwa sauti!
@emu three pamoja sana wangu@Simon nimekubali sana tuko pamoja.
Chapisha Maoni