Alhamisi, Desemba 09, 2010

Swali kutoka kwa Halima mkazi wa Arusha "Mume wangu ana tabia ya kusimulia siri za ndani ya nyumba kwa majirani na marafiki zake.

Jamani hivi ni kwa nini unakuta baadhi ya wanawake au wanaume wanakuwa na tabia ya kutoa siri za mambo ya majumbani mwao?? ,,Halima mama wa watoto wanne anaomba ushauri anasema "imekuwa ni hali ambayo inajirudia sana katika maisha ya ndoa yangu kwani hii tabia yamume wangu imenichosha akikaa  na marafiki zake anazungumza nao mabo ya nyumbani mengine yakiwa ni ya aibu kwani huzungumza hadi mambo ya chumbani,sasa mimi nikiwa katika mizunguko hayo maneno nayapata kiukweli hii hali inaniuma sana na kila nikimueleza basi inakuwa ni ugomvi hata kunipiga ananipiga na akinipiga lazima atawasimulia majirani nimechoka na hii hali sijui nifanyeje naomba ushauri kutoka kwa watu mbalimbali......

Maoni 4 :

Bila jina alisema ...

Thought unahadithia from your own place,kumbe bado uko kwake?kweli unampenda..vumilia au mpeleke kwa psychologist!

Bila jina alisema ...

Ongea nae inaweza saidia, mwambia watu wanasema vibaya, manakua gumzo la mji, kuachana no, ni kitu kikubwa ofcourse bt si kwa extent ya kuachana

emu-three alisema ...

Kutokujua nini maana ya ndoa kunachangia sana kuharibu ndoa kwa matendo yenu wenyewe. Ndoa ni kitu cha thamani na kitakatifu, kina msharti yake, na mojawapo ni kuwa siri za wandnoa ni baina ya wanandoa wenyewe. Tukisema siri ina maana yale mambo ya faragha!
Ukiona mwandoa anabwabwaja hayo kwa wenzake, ama ana walakini na inabidi wataalmu wamhakiki, au ndio ujinga wa kutokujua nini maana ya ndoa. Na ndipo tunapoona umuhimu wa vitu kama Kitchen party,ambayo hufanywa kwa wanawake tu, hii ilitakiwa na mwanaume ashirikishwe.
Ni vyema kabla ya watu kuingia katika ndoa kuwe na madarasa ya jinsi gani ya `ndoa' kwanini na masharti yake. Haya yangefanywa na wanadini, au hata hawo makungwi, ingawaje wengine hopotosha kwa mfano wa mafiga matatu nk.
Huyu mwanandoa anayetoa siri...sijui tumuiteje..ikishindikana muite kiongozi wako wa dini ampe darasa...inasikitisha kama wapo watu wa namna hiyo...kwani anadhalilisha dhana nzima ya ndoa. Hebu muulize atasikiaje akikuona wewe unatembea uchi barabarani? akikujibu kuwa haiwezekani atakuchukulia hatua muulize je hayo anayoyahaidthia mitaani haoni kuwa anakuweka uchi barabarani?

Bila jina alisema ...

MWELEZE KUWA TABIA YAKE WEWE HUJAIPENDA NA KWA NINI AWE MSHAMBA WA MAPENZI KILA ANACHOFANYA NA MKEO HAKISTAHILI KUSIMULIA WATU

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom