Jumatano, Desemba 01, 2010

Unapogundua mwenza wako anakusaliti ni vyema kutafakari ili kuchukua maamuzi sahihi.

Rihana na Chrisbrown pichani enzi za uhai wa penzi lao kwa sasa kila mmoja anaendelea na mambo yake, katika mapenzi kuna mambo mengi huwa yanatukia hasa linapokuja suala la usaliti inapotokea mwanamume au mwanamke kumsaliti mwenza wake chanzo ikiwa ni tamaa,migogoro na mambo mengine mengi sasa inapotokea unagundua kuwa mwenzio anakusaliti ni vyema ukatafakari kwa kutulia kwani ukikurupuka kwa hasira unaweza kufanya mambo ambayo yatakusababishia matatizo zaidi. 

 Mfano tukio lililotokea huko Kagera katika kijiji cha Kumwendo kata ya Mbuga likimuhusisha mtuhumiwa Oswald Bilimdi mwenye umri wa miaka 50 kurusha bomu katika nyumba ya William na kusababisha kifo cha Philemon Ngaingeza  na baadhi ya watu kujeruhiwa. chanzo ikiwa ni baada ya mtuhumiwa  kumtuhumu marehemu kufanya mapenzi na mke wake hadi kuzaa naye mtoto mmoja.mtuhumiwa anashikiliwa na polisi huku upelelezi ukiendelea.Matukio kama haya yanayosababishwa na wivu wa kimapenzi yanatokea sana na watu kujikuta wakifanya mambo ya hatari ni muhimu kutafakari kabla ya kutenda.

Ni kweli inauma ukigundua mwenza wako anakusaliti lakini kumpiga au kuua sio njia sahihi ya kutatua matatizo ila ni kuongeza matatizo.

Maoni 3 :

Bila jina alisema ...

mtu anakufatilia sana mara uchunguzi huu mara ule, cha kushangaza akishakamilisha uchunguzi wake mbona haachi? sasa kumbe anachunguza ili nn?

na wengine kubambika kesi kwa wapenzi wao ndo wenyewe. sasa ili iweje? wanaboa

Bila jina alisema ...

mtu anakushutumu ooh ww malaya lakini anakung'ang'ania, ukimwambia km vp aachie ngazi hataki, sasa huwa najiuliza ina mana anapenda kuwa na malaya, au basi ni kwa vile kaamua kukutusi. mh

Bila jina alisema ...

mmh!... hawa maanonymous wana vituko! mbona maoni yenu hayahusiani kabisa na habari yenyewe?? Adela anaongelea jinsi ya kuwa mtulivu baada ya kugundua unahujumiwa katika penzi. kama unaitwa malaya na mpenzio na wakati hujafanya chochote kusababisha mwenzi wako kukuita hivyo basi ana matatizo huyo!! ila nakushauri ufikiri sana kwanini kafanya hivyo..

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom