Jumanne, Septemba 28, 2010

Katika maisha unavuna ulichopanda,,iwe shuleni,kazini au popote pale,,usijibweteke.

Huyu ni mwanafunzi yupo darasani kwa umakini akiwa anaandika,,ukiwa shuleni unakutana na vikwazo au vishawishi vingi lakini ukijitahidi na kujua nini unakitaka ili kufikia malengo yako lazima utafanya vizuri na kufaanikiwa,kama ulikuwa na ndoto za kuwa mwanasheria,,Daktari nk.. inawezekana kwa juhudi zako..mzazi msaidie kijana wako kufikia malengo yake  kwani vishawishi wanavyokutana navyo ni vingi hususani mtoto wa kike.......


Maoni 2 :

Hashir alisema ...

Nikweli kabisa dada yangu, waswahili wanasema, mchumia juani hula kivulini, hii inamaana kwamba ukihangaika kutafuta kwa shida basi utafaidi matunda yake hapo baadae kwa raha, kijana unatakiwa uhangaike na maisha yasikutishe wala hutakiwi kukata tamaa, jitahidi kujipanga na kujishughulisha kwa yaliyo mema na halali kwako ili baadae uvune mavuno mema!

ADELA KAVISHE alisema ...

@Hashir asante tuko pamoja dunia hii bila kuhangaika huku ukiwa na malengo ni vigumu sana kufika,,,na pia muhimu kujitambua,,na kuepuka vikwazo na vishawishi

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom