Ubunifu katika mapenzi ni ile hali ya kujaribu kuleta vitu tofauti katika mahusiano baina ya wapendanao,ili kufanya penzi kuonekana jipya kila wakati,tazama picha hii huyu kaka anamsaidia mwenza wake katika mapishi huku wote wakiwa na furaha,inawezekana mwanamke ni jukumu lake kuandaa chakula lakini katika suala la ubunifu mwanaume naye anaweza kuamua siku moja kumuandalia mwenza wake chakula ili kuleta ladha tofauti, kwa kuamua yeye mwenyewe inapendeza sana.. |
| |
Inawezekana ukafanya hivi pia ukapamba kitanda chako vizuri ukaweka maua mazuri pamoja na mvinyo kama unavyoona kama huwa mnatumia mwenzio akirudi kutoka kazini na kukuta mabadiliko kama haya mara mojamoja inampa faraja na kuona hakuna kama mke au mume wangu,,Ubunifu huu unaweza kuwa katika sehemu mbalimbali katika mapishi, maongezi, mavazi, urembo,maendeleo nk. Ni jukumu lako kuwa mbunifu wakati wote ili kuongeza mvuto katika penzi lenu.... |
Maoni 1 :
.....kwa wengine utaonekana kama vile unajikomba! Hivo inabidi ulichukulie kwa umakini kabla hujaanikwa mtaani kwa mashostito na mablazameni kuwa 'yule kadata, anajikomba kwa kuniletea hiki ama kile'... :-(
Chapisha Maoni