Alhamisi, Oktoba 21, 2010

Kula kiasi ili uwe huru kwani kushiba sana kunaleta uvivu.

Ukila kupita kiasi  wakati mwingine unaweza kusinzia na kushindwa kufanya kazi vizuri,hapo Chipsi kidogo,tambi maharagwe na mishikaki kwa mbali uache kunenepa tu,nilimkuta mdogo wangu akiwa anajipatia chakula hicho hapo juu.ni mchanganyiko ambao ukiuendekeza duuh unaweza kuongezeka mwili kwa haraka sana.


Hapo Alice Kavishe akiwa anajiachia akiwa ameanza kushiba safi kabisa ,,jamani kwenye chakula hakuna aibu kama una njaa kula unavyoweza lakini usizidishe kipimo



Hapa kazi imeisha kachoka hoi na tabasamu kubwa baada ya kushiba huku akiwa ameshikilia maji ya Kunywa,jamani wataalamu wanakuambia usinywe maji wakati ukiwa unakula,baada ya kula ikipita kama nusu saa ndio unatakiwa kunywa maji sijui kama waliowengi wanaweza kufanya hivyo..ni hayo tu jipendelee kwenye maakuli mwenzangu usijinyime.



Maoni 5 :

emu-three alisema ...

Kweli kila kitu kina mpaka wake, usile sana au kufanya kitu kupita kiasi.
Mhh, huyu mdogo wako, wote mpo bomba sana. Hongereni!

Yasinta Ngonyani alisema ...

Heh! Adela nimeona umefanya badilisho la picha hapo juu bombi kweli. Haya sasa tuje kwenye kula ni kweli kabisa kula mno ni hasara, maana utakuta kuna wakati mtu unakula kwa sababu chakula ni kitamu sio kwa vile una njaa hapana. Na baadae utakata mtu kachoka sasa hapo kuna maana gani, hii hata chakula cha jioni wengi wanafanya kosa wanakula chakula cha jioni saa tatu-nne usiku hii si nzuri kwani huwa inaleta shida sana wakati wa kulala. Usingizi inakuwa shida kuupata kwa vile tumbo linakuwa bado limejaa.Kwa hiyo kwa afya inabidi kula chakula cha jioni baina ya saa kumi na moja jioni mpaka saa kumi na mbili......

EDNA alisema ...

Kweli watu tunatakiwa kula kwa kipimo jamani, sio mtu unakula mpaka unavimbiwa mweeeeee.Kadogo kako kamependeza kama dada yake...so cuuuute.!!

ADELA KAVISHE alisema ...

@Emu three thanx wangu @Yasinta asante mwaya ujumbe umefika my dia tuko pamoja@Edna thanx pia dia wangu.

o'Wambura Ng'wanambiti! alisema ...

inategemea unakula chakula gani, hai ama kilichokufa! Chakula hai hakina madhara sana kama kile kilichokufa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom