Pages

Ijumaa, Oktoba 01, 2010

Matukio ya hatari katika mahusiano alipiza kisasi kwa mumewe kwa kumkata uume akidai amemuambukiza Ukimwi..

Inawezekana matukio kama haya katika picha hii huwa yanatokea mara kwa mara mwanamke kumpiga mwanamume,,au mwanamume kumpiga mwanamke na chanzo ikiwa ni migogoro inayotokea katika mahusiano...
Katika tukio lilotokea huko Kiwalani,,mwanamke mmoja Bi.Halima Thomas(28) amefikishwa katika mahakama ya Ilala kujibu mashtaka ya kumkata uume mume wake.

Baada  ya  kusomewa mashtaka, mshtakiwa alikiri kufanya kosa hilo  akidai kuwa amefanya hivyo kwaajili ya kumkomesha mume wake ambaye anadai kuwa amemuambukiza Ukimwi..tena akaongeza kwa kusema "nasikitika kwa kumkata kidogo ule uume ningejua ningeumaliza kabisa ili usifanye kazi tena kwani ataendelea kusambaza Ukimwi kwa wanawake wengine" Alidai mshtakiwa.

Mshtakiwa yupo Rumande na kesi itatajwa tena oktoba 12 mwaka huu..
Hatari hii jamani,,Je kwa kufanya hivyo huyo mwanamke alikuwa sahihi kweli,,,mmmhh..ngoja niwasikilize wadau...

Maoni 2 :

  1. kwa utu alichofanya kwa kweli si haki ila tu ilibidi afanye hivyo kwa kushikwa na hasira. Kwa sababu wakati mwingine mtu unaweza kukasirika na kufanya kitu ambacho hukupanga. Ila duh! pole sana.

    JibuFuta
  2. @Yasinta asante kipenzi yaani katika hali kama hiyo kiukweli huyu dada alipatwa na hasira sana,na hata kwa yeyote yule kutokana na hasira mtu unaweza ukajikuta umechukua uamuzi ambao unakuingiza katika matatizo..

    JibuFuta

Unakaribishwa kutoa maoni yako.