Jumatatu, Oktoba 11, 2010

Ni muhimu mwanamume kujipenda na kupendeza,,kumbuka mavazi pia yanaelezea mtu alivyo.

Mavazi unayovaa hususani katika maeneo ya kazi yanakuelezea jinsi ulivyo kabla wewe mwenyewe kuzungumza neno lolote,kwani yanaweza kumfanya mteja wako katika biashara au kazi atarajie nini kutoka kwako,kama utavaa vizuri ndivyo utakavyofanya vizuri katika kile unachokifanya,ukivaa vibaya huwezi kuwa huru katika kazi yako,unaweza kupoteza wateja wako katika makubaliano ya kibiashara,kukosa mchumba au hata kukosa kazi pale unapotafuta ajira kutokana na muonekano wa mavazi yako.


Kupendeza hakuangalii umri wala umbile alimradi uwe makini katika uchaguzi wa mavazi yanayoendana na wewe,kama utakuwa ni mtu unayejipenda na kujiweka vizuri na matokeo yako yatakuwa mazuri,lazima uwe mtundu na unayependa kwenda na wakati ili kuongeza vidokezo katika utanashati wako mwanamume.
hivi ni baadhi ya vitu muhimu katika mavazi ya mwanamume ,mwanamume anatakiwa awe amevaa saa nzuri ya mkononi,Tai nzuri iliyo na rangi zinazopendeza na kuendana na shati lako isiwe na maua mengi sana,viatu vya ngozi na soksi,usivae raba sehemu ya kazi haipendezi inategemea na kazi na suruali uliyovaa kama ni ya kitambaa inapendeza kiatu cha ngozi ,,pia viatu viwe vyeusi au kahawia,usivae kiatu cha njano au pink sehemu ya kazi labda uwe ni mcheza shoo au msanii,kumbuka kuvaa soksi safi na viatu viwe visafi wakati wote zingatia usafi wa mavazi yako.hiyo ndiyo inakuwa siri ya mavazi kwa mwanamume.

Maoni 1 :

Bila jina alisema ...

" ...kumbuka mavazi pia yanaelezea mtu alivyo" Upande gani ni mzito zaidi? Kwenye tabia au utanashati wa mtu. Kwa sababu ni uamuzi wa mtu binafsi labda kwa ajili ya kuonekana au kutofungwa na hivyo dhamira. Japo inaukweli hasa ukieleza ubadilikaji wa kitabia katika shughuli au hali fulani. Lakini sio kuonesha kuwa mtu huyu yuko hivi hasa akivaa hivyo kwa sababu mara nyingi mtu atavaa mavazi mazuri kwa ajili ya kitu fulani. Mfano sherehe, au hafla fulani hivi, mtu lazima atavaa nguo nzuri. Hiyo lazima iwe ni dhamira ilikubalika kutokana na mtu kuona hamna jinsi.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom