Jumanne, Oktoba 12, 2010

Tumia vitu asili kwa ngozi yako...

Ili ngozi iweze kuwa na mvuto inahitaji matunzo,ngozi inayoachwa bila matunzo kamwe haiwezi kuwa na mvuto,ngozi inaweza kutengenezwa kupitia vipodozi vinavyotengenezwa na kemikali mbalilmbali,lakini pia inaweza kutunzwa kupitia viasilia mbalimbali vitokanavyo na mimea au mazao ya shambani,,

Matunda ya aina mbalimbali yanasaidia sana katika kutunza ngozi yako.matunda kama Tango na maparachichi hutumika katika kutunza ngozi kwa kula pamoja na kupaka usoni,,pendelea kula aina hii ya matunda na pale unapopata muda chukua tango lako lipondeponde changanya na mayai na alovera kisha zisage vizuri baada ya hapo paka usoni,shingoni au popote mwilini,,subiri dakika 20. baada ya hapo safisha uso wako unaweza kufanya hivi mara kwa mara kila wiki.ili kutunza ngozi yako.na ikishindikana waone wataalamu wa masuala ya ngozi kiutaalamu zaidi.


Maoni 7 :

Yasinta Ngonyani alisema ...

Adela! ahsante kwa darasa hili zuri, Nimeprint nitajaribu.

ADELA KAVISHE alisema ...

poa kipenzi @Yasinta ni nzuri sana..

EDNA alisema ...

Asante mdada,tutafuata ushauri wako...ila mimi ngozi yangu ni ya mafuta sana nini nitumie nipunguze mafuta? kama unajua tafadhari tuambizane.

Mzee wa Changamoto alisema ...

Ahaaaaaaaaaaaa!!!!
Kwa bahati mbaya iliyo nzuri NIMEWASILI HAPA
Na nimekutana na habari murua
Karibu kwenye ulimwengu wa ku-blogu dadangu. Twawahitaji wengi zaidi
Baraka kwako na asante kwa shule nzuri

Simon Kitururu alisema ...

Ohoo Bibi yangu akiwaona mnajipaka matunda atawafinya kwa kudhani mnachezea chakula nyie shauri zenu!.:-)

ADELA KAVISHE alisema ...

@Edna poa my dia usijali tuko pamoja@Mzee asante pia tuko pamoja@Simon hahahahaha hatuchezei tunatumia kutunza ngozi..

Bila jina alisema ...

Adela mm nakupenda sn km huna mume au mchumba hebu tuwasiliane.

Magulu
Masomoni
Germany

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom