Jumatatu, Novemba 29, 2010

Bora kuwa mpweke kuliko kuishi na mtu usiyempenda

Katika mapenzi kuna tatizo kubwa ambalo unaweza kukutana nalo usipokuwa makini pale unapokuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na mtu usiyempenda au ambaye hakupendi lakini wewe unalazimisha wakati mwenzio hakupendi na yupo na wewe inawezekana kwasababu ya jambo fulani.sababu kubwa inayosababisha mtu kuwa na mwenza asiyempenda ni pale anapofikia maamuzi ya kuwa na mpenzi kwasababu hataki kuwa peke yake au anataka kuolewa kutokana na kuona umri unasogea hivyo anaona bora awe na yeyote yule bila kujali anampenda au la pia pesa inaweza kusababisha kuamua kuishi na mtu usiyempenda  .

Kumbuka kufanya maamuzi sahihi katika mahusiano kwani kulazimisha kumpenda mtu wakati haumpendi au kujilazimisha kwa mtu asiyekupenda ni jambo ambalo mwisho wake huwa mbaya na kujikuta unakuwa mtumwa wa mapenzi....JENGA UTAMADUNI WA KUJIAMINI NA EPUKA KUWA MTUMWA WA MAAMUZI YA KILE AMBACHO HUKIPENDI BASI NI LAZIMA KUWA WAZI NA USIWE UNAOGOPA KUWA NA MAAMUZI SAHIHI.

Maoni 4 :

Yasinta Ngonyani alisema ...

"Bora kuwa mpweke kuliko kuishi na mtu usiyempenda" Adela umesema kweli kabisa nimeupenda msemo huu.

gmkilalu@yahoo.com alisema ...

Mwanangu ni kweli kabisa

Bila jina alisema ...

haswaaaa... wengine wanaboa mbaya, m2 mwingine anakung'ang'ania kuliko luba, mm nashindwa kuelewa mwenzenu. coz km kumwambia tayari lkn bado tu m2 anang'ang'ana pamoja na vituko vyote wala hashtuki. eti coz marafiki, ndugu, wanajua yuko na mm, INAHUSUU........

Bila jina alisema ...

kweli hata mimi naunga mikono na miguu b est

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom