Jumapili, Novemba 28, 2010

kuwa mbunifu kwa kumuandikia ujumbe mzuri wa kimapenzi mwenza wako,na haipendezi kutumia majibu ya mkato kujibu ujumbe kutoka kwa mwenza wako.

Maneno hayo pichani ni ujumbe mzuri sana wa kimapenzi kwa wapendanao maneno kama nakupenda sana,wewe ni kila kitu kwangu wewe ni ndoto yangu nk, na maneno mengine mazuri na matamu yanapendeza sana kutumika mara kwa mara kwa yule umpendaye lakini wengi wao hujisahau baada ya mazoea kwani inawezekana mwanzoni mwa uhusiano wenu mlikuwa mnatumiana sana ujumbe mzuri wa kimapenzi lakini baada ya kuingia kwenye ndoa  mazoea yanazidi hadi mnajisahau kama mnatakiwa kuonyeshana mahaba ya dhati zaidi..unaweza kuona ni kitu kidogo lakini kina maana kubwa sana katika mapenzi.

Ujumbe wa kimapenzi hauangalii mwanamke au mwanamume yeyote anaweza kuandika kwa mwenza wake ijapokuwa mara nyingi unakuta wanawake ndiyo tunaangaika zaidi katika hili na wakati mwingine mtu unaweza ukawa umejipinda umeandika ujumbe mzuri wa kimapenzi kwa mwenza wako lakini yeye akakujibu kwa kifupi sana mfano ok,yes me too,,take care nk. kitu ambacho kiukweli inaumiza kwa upande mwingine sasa sijui ni kuwa bize au ni mapozi,,ila ni muhimu kuwa mbunifu ili kuimarisha penzi lenu milele.

Maoni 4 :

Hashir alisema ...

Daah! hapa kweli umesema jambo, yaani hii tabia ibakera saana, halafu inaleta maswali mengi tu baina yenu, coz kama mwenzio kakuandikia message nzuri, haifai kumjibu kimkato mkato as u said, pia kunatatizo la kuchelewa kujibu message, utakuta mtu unamtumia message, halafu anakaa muuuuuda mrefu kujibu, ukimuuliza utasikia aaaaaahhh nilikuwa nime concentrated sana kwenye movie ndiomaaa, mmmmh inamaana movie na msg yangu basi jamani daaah! si freshi kabisa vijitabia kama hivi....

Simon Kitururu alisema ...

Mmmh!

Bila jina alisema ...

Mh my dia, eti mwanaume anauliza oohh mbona cku hizi hutumi msg nzurinzuri, mm nikampa adhabu, nomba na ww unitumie msg nzuri, till yet hajatuma k2. sasa mm nashangaa sana hawa wa2 wanaopenda kufanyiwa v2, yani ina cc wadada ndo tunajua sana kupenda ama hawa wanaume ni ubabe tu. sielewi.

Gg

emu-three alisema ...

Mhh, nakumbuka nilituma kitu hapa, ok well labda mtandao haukunasa. Ujumbe ni makini, na upo wazi!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom