Jumamosi, Novemba 27, 2010

Kwa nini baadhi ya wanawake wanafunga ndoa wakiwa tayari wamebeba ujauzito.

Kiukweli kwa mtazamo wangu kwa sasa nimeshuhudia akinadada wengi wakifunga ndoa tayari  wakiwa ni wajawazito na kutoka na uchunguzi niliofanya ukiwauliza wanaume wanakuambia lazima ujaribu kwanza kama mwanamke anauwezo wa kupata mtoto au la,wengine wanasema inakuwa ni bahati mbaya,au unakuta imetokea binti amepata ujauzito na hivyo kutaka pindi atakapopata mtoto awe ndani ya ndoa, na wanawake waliowengi wanasema inabidi kuangalia kama nitapata mtoto ili kuepusha maneno kwa ndugu wa mume.majibu yalikuwa yanatofautiana lakini mimi nikaona ni kama kutokujiamini kwa mawazo kama hayo .


Mwanamuziki Alicia Keys pichani wakati wa harusi yake alikuwa ni mjamzito, na kuna wengine wengi wakiwemo watu maarufu na wasio maarufu kipindi hiki wanafunga ndoa mwanamke akiwa ni mjamzito.je ipo sawa hii mdau au kwa upande wako unasemaje


Maoni 3 :

Yasinta Ngonyani alisema ...

Nafikiri inatokea tu au labda wanapenda. Ila hiyo ya kusema eti wanajaribu kwa kweli napingana nayo kwani inaonekana kama hakuna penzi hapo. ETI KUJARIBU mmmhhh!!

Bila jina alisema ...

wengine bahati mbaya, wengine mr anakupima kwanza no ndoa bila mimba, kina dada nasi tunadhani tukibeba mimba ndo tutaolewa,wengine wana hamu ya mtoto, just sielewi elewi. tuone na wengine.

Gg

Bila jina alisema ...

mimba kwanzaa ndoa badayee ndo mpango mzima siku hizi

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom