Pages

Alhamisi, Desemba 09, 2010

Inawezekana mwanamke akawa ni mzuri mwenye kila sifa ya kuolewa lakini asiolewe je ni kwanini,

Katika maisha unweza kumkuta binti mrembo lakini akawa hana bahati ya kuolewa labda kutokana na tabia,,na mambo mengine,,but i need to know ni kwanini huwa inakuwa hivyo naomba niwasikilize wadau.

Maoni 4 :

  1. Ndoa si bahati kama wengine wanavyodhni. Pia si uzuri wa umbo na sura peke yake. TABIA ni jambo kubwa sana ambalo watu wanalishau mno. Pia si wanawake wote wanapenda kuolewa haraka haraka wanaona wamalize kila kitu waolewe. Celine Dion kwa mfano kaolewa akiwa mtu mzima tu wakati ni mzuri na alikuwa na hela za kumwaga. Sasa ana miaka 42 na kazaa watoto mapacha wazimaaaa. Kwahiyo, pande mbili zote ni factor changizi.

    JibuFuta
  2. wanaume wengi wanawaogopa wanawake wazuri, huwa wanadhani labda wakiwafata kuwaaproach watabwagwa, wanadhani wanawake hao wazuri may b lazima hawezi kuwa cngle yani anahisi tayari ana m2. wanajickia, wanaringa, nk. kumbe wapo wazuri wataratibu tu,wapole, wenye adabu.

    nawaomba wanaume WAJIAMINI TU, c ajabu wanawake wazuri wengi wapo cnlge.

    JibuFuta
  3. Mwanamke yeyote anayejiona ni mzuri huwa anajisikia sana na kuwa na makeke fulani.Pia mzuri ni soko la watu wengi hivyo wanaume wanaogopa kuchangia na watu wengi wawaoapo.Lakini kikubwa ni kwamba wengi wanaume wanadhani akioa mwanamke mzuri atakuwa kwenye shida ya ndoa kwa sababu mke wake atakuwa anatongozwa na watu wengi sana.Hao wazuri wengi hawaachi kujivuna na ndiyo maana wanabaki single milele na kuishia na mapenzi ya mitaani.

    JibuFuta
  4. Kwa mtazamo wangu mimi, uzuri wa mwanamke sio sababu ya sisi wanaume tulio wengi kuwaogopa kuwa approach kama wanavyo dai watu wengi lah! ila wanaume kwa kiasi kikubwa ndio watafutaji wa pesa, achilia mbali hizi kampeni za sasa za uwezeshaji wa wanawake. hivyo basi kutokana na hali ngumu wanaume ambao ndio watafutaji wamegundua hasara kuliko faida, kwani hawa wanawake warembo ni sawa na gari ya thamani, wana gharama. sasa kwavile service ni ileile kama ya huyo mwanamke mrembo, watu wanaenda kwa hawa ambao mimi nawata ni warembo zaidi ya hao(hawatumii ziada juu ya urembo wao), kwani ndoa sio urembo na gharama bali ni mapenzi, huduma na hatimae mazao ya ndoa yaani watoto. so kama wote wanazaa, wanamapenzi na msaada why uingie gharama zisizo za lazima? Waache hao warembo waishi wenyewe, najikuna ninapo paweza. byeeeee!!

    JibuFuta

Unakaribishwa kutoa maoni yako.