Picha ya mama akiwa anafanya kazi huku amembeba mwanaye.,, haya jamani hili suala la baadhi ya kina baba kutaka mwanamke awe mama wa nyumbani nilizani siku hizi hakuna kwani siku hizi wanawake tunatakiwa kuchakarika lakini kumbe yapo bado,,Mayasa amesema mume wake ni mfanyabiashara na uwezo wa kifedha anao sasa anataka mke wake ambaye ni mwalimu aache kazi ili awalee watoto nyumbani kwa madai kuwa mahitaji yote yeye ndiye hutoa pale nyumbani na kutokana na hilo kila kukicha ni ugomvi baina ya Mayasa na mume wake ambaye hataki housegirl awalee watoto wake watatu mmoja mkubwa ana miaka 7, mwingine miaka 5, na mdogo ana miaka 2 ...je unamshauri nini mdau....... |
Maoni 7 :
Huo ni mtihani maana yupo mama yangu mdogo aliambiwa hivyo akaacha kazi baadaye ikatokea sintofahamu baba huyo akamuacha mama mdogo, na mpaka leo mama mdogo huyo hajapata kazi!
Kitu muhimu ni kukaa na kuongea, na kupeana ushauri, mpime muone faida na hasara zake, na ikibidi , basi muandikishane, kuwa sasa naacha kazi ikitokea la kutoe, hiki na hikii kiwe wazi.
Ndoa ni muhimu sana, na wajengaji na wavunjaji ni wanandoa wenyewe. Kazi ni moja ya kusaidiana, kama kazi itasababisha kuvunjika kwa ndoa, inabdi kuangalia kipi bora, kazi au ndoa?
Hapa ni mtihani. Ila kaeni mliongelee tena, hata ikibidi wahusisheni wakubwa, mliweke sawa!
DADA,SIO KWAMBA NAKUFUNDISHA KIBURI BUT FOR THE SAKE OF YOUR KIDS..USITHUBUTU KUACHA KAZI..MAISHA YA SIKU HIZI YAKO TOFAUTI NA YA ZAMANI, LABDA MUMEO HAONI USAIDIZI WAKO KATIKA FAMILIA UNAOTOKANA NA KAZI YAKO BUT NAAMINI IPO SIKU ATAONA NA ATAKUSHUKURU..
WAHUSISHE WAKUBWA ILI UMUELEZE MUMEO NI KWA KIASI GANI KAZI ULONAYO INA MANUFAA KWA WOTE WAWILI NA FAMILIA YAKO...
Huna sababu ya kuacha kazi. Kama mwalimu jamii inahitaji huduma yako. Pia una muda mwingi wa kukaa na watoto wako baada ya kazi. Kazi yako itakusaidia enapo atakuacha mumeo, akipata tatizo utaweza kumsaidia.
kukaa nyumbani bila kazi inaboa sana.
Fanya kazi, ongea na mumeo taratibu umweleze sababu za wewe kuendelea kufanya kazi si mahitaji tu.
swali:- kwa nini wasiwapeleke watoto chekechea? na hapo wote watafanya kazi kama kawaida.
duh! hii tena kali lakini haileweshi.
mie naona kaa na mumeo uongee nae kwa adabu, km vp mshirikishe wakubwa, yani my dia kukaa home kunaboa sana. dada yangu amesoma tena ana fani 2 ya unesi na Ofc management,alivyohitimu tu akaolewa. mume ana kila k2 lkn jamani hadi hela nauli ya kuendea kkoo uombe. basi dada yangu ni kukondeana tu, hana raha. ujue hakuna m2 chake bana, mali iliyo mfukoni kwa mwenzio haikuusu hata kdg.
jibu. watoto wakienda chekechea kwani c lazima hawatarudi nyumbani
Chakusikitisha ni jinsi BINADAMU wenye akili wafikiriavyo kwa ufinyu mahitaji ya BINADAMU mwenye akili.
Kama pesa ingekuwa ni maana ya maisha ya BINADAMU. Matajiri kama akina Bill GATES wasingekuwa wanaenda kazini kila asubuhi kwakuwa Bill gate mtu mmoja ana hela kuliako nchi zote za AFRIKA MASHARIKI.
Mahitaji ya BINADAMu ni mchanganyiko wa mengi na ndio maana katika mchanganyiko mwingine unaweza mpaka kumshangaa umheshimuye kusikia eti pamoja na yote YA KIHESHIMA na mafanikio yake ila bado anaamini MBUYU kwa kuwa pamoja na yote hana furaha kuna kitu kimepungua.
Mwnamume afikiriaye kwa kuwa anaweza kulipia yote ya MKE wake anasahau kuwa MWANAMKE wake ni MTU kwa kuwa kama MTU kiutu inabidi utulize mishawasha ya utu kama MTU.
hivi bado watu wanashangaa ni kwanini akina MADONA wenye pesa zote hawana FURAHA?
Wenye MADEMU au WAUME wazuri bado wanagawa nje?
Wenye YESU wanachunguza ya MOHAMMEDI?
Wenye pilau wanawaza UGALI wa MUHOGO?
Ni vibaya kupunguza ya MTU na kufikiria KITU kinatibu yote kisa unafikiri MTU ni ni simple hivyo na kwa kuwa unampa BENZI na makabrasha kibao maana yake umemtibia kila kitu na kwa hiyo yako ndio yawe yake.:-(
Nawaza tu!
Chapisha Maoni