Pages

Jumatatu, Januari 30, 2012

Siyo kila unachokiona ama kukisikia lazima ukiseme wakati mwingine bora unyamaze kuliko kusema.

Kuna baadhi ya watu wanatabia kila anachokisikia basi lazima akiseme yaani anaona taabu sana kukaa nacho moyoni lazima aseme roho yake ndiyo itulie,,mimi naamini kuna vitu vingine si lazima kusema  wakati mwingine mtu unatakiwa kujifunza kukaa kimya kwa mfano labda umekutana na mtu haumfahamu unaona amevaa nguo rangi azijaendana basi unaanza moja kwa moja kumuambia hajapendeza yaani vitu hata havikuhusu na wakati mwingine kunyamaza kimya kunaepusha shari,, mfano mwingine unakuta wamekaa marafiki anatokea mtu na kuanza kumsema mume wake ama mke au ndugu yake yeyote mbele ya marafiki zake,, na wakati huo mtu huyo unayemsema hayupo bila ya kujua moja kati ya wale unaowasimulia wanaweza kwenda kumuambia unayemsema pia kuna tabia ya watu kuwasema wenzao maumbile yao ,,magonjwa wanayougua nk kitu ambacho hakileti maana ni bora kukaa kimya kwa mambo yasiyokuhusu.

Kuna baadhi ya watu pia anaenda kwa rafiki amealikwa basi ataanza kukosoa nyumba, chakula alichopewa kana kwamba yeye anajua kila kitu sasa hali kama hii inaweza kukusababisha ukakosa marafiki kwa kuropoka na mambo mengine yasiyokuwa na maana. BORA KUNYAMAZA KULIKO KUSEMA YASIYOHUSU.

Maoni 5 :

  1. Adela haya maneno ni kweli kabisa jamani kwani kuna watu wanaropoka sana bora kunyamza siyo kila kitu kusema

    JibuFuta
  2. jamani ujumbe umefika lol watu wengine midomo yao iko juu kila wakati

    JibuFuta
  3. kuna mtu fulani namfahamu anayo hii tabia inakera sana

    JibuFuta
  4. Sometimes inabidi uwe Zipped

    JibuFuta
  5. ila kweli ya baki palepale kwamba hata kama hujisikii sema ila lugha ya mwili itazungumza kwamba unasema nini

    JibuFuta

Unakaribishwa kutoa maoni yako.