Pages

Jumanne, Agosti 28, 2012

Anaomba ushauri wadau "mpenzi hataki kumuona wala mimba aliyompa haitaki"

Mimi ni msichana ambaye nilikuwa na mpenzi ambaye hatuna  muda mrefu sana, tulipanga mipango mingi na mizuri sana, kwani pia tulipanga kuoana kabla hajaenda masomoni nje ya nchi,,  lakini pia kutokana na kwamba alikuwa ananipenda aliniambia inabidi aniache na ujauzito ili nisimsaliti na mimi kwasababu nampenda nilikubali kwahiyo baada ya muda nilipata ujauzito na tulienda wote nikapimanakugundulika kuwa nina ujauzito alifurahi sana, lakini baada ya muda kupita nilimkwaza sana mpaka akanipiga na niliendelea kumkwaza kwa message chafu pia nikamwambia kuwa natoa mimba

 Nilikuwa nikimwambia yote hayo kutokana na hasira ya kipigo alichonipa, baada ya siku chache nilifikiri hali ingerudi kuwa kawaida lakini kumbe m amekasirika hadi leo hataki hata kuniona nimejaribu kumuomba msamaha amekataa na hata nilipotafuta watu wazima waniombee msamaha amekataa pia na kusema kuwa harudi nyuma, na pia amenikataza nisimpigie simu na mimba haitaki na mimi moyoni bado nampenda nasiwezi kulea mimba ya mtoto asiye na baba nahisi kama nachanganyikiwa sijui nifanyeje naombeni ushauri

Maoni 5 :

  1. we ni mtu mzima kweli?kuolewa kwani mbaka uwe na mimba?si angekuoa tu kama anakuoa, changamsha kutoa hata kama miezi mingapi utajuta kulea mtt asiye na baba acheni ujinga watoto wa kike

    JibuFuta
  2. Akae asubirie ajifungue salama aone mtoto anafanana na nani inaweza kuwa huyo boyfriend amuamini. Vumilia tu dada.

    JibuFuta
  3. ungetuambia umemkwaza nn hasa ndio tungekushauri

    JibuFuta
  4. Wahenga na wanadini walipotushauri kuwa ni vyema kuoana kwanza kabla ya mimba waliyajua haya. Haya ni matokea ya kukaidi mawaidha ya ushauri wa wakubwa. Pole sana.

    Lakini maji yameshamwagika huwezi tena kuyazoa, ni nini kifanyike;

    KWANZA, tubu, na muombe sana mungu wako, PILI uwe na SUBIRA,kwasababu hapo ulipo upo kwenye mtihani wa kulea mimba, usijitwike mizigo mingine,mengine ni majaliwa.

    NA TATU Usirejee makosa hayo tena.

    Je itakwuaje, je mapenzi yapo, je..je je? maswali mengi kwa sasa sio muhimu sana.

    Ukumbuke kuwa mlikuwa hamna mkataba wowote,na mkataba halali ni ndoa,nyie mliamua kupimana kwanza, na hayo yameshatokea, kwahiyo mengine yote yatategemea huyo mwenzako je kweli alikuwa akikupenda, au nia yake ilikuwa kupata hicho alichokitaka!

    Mtoto ni moja ya jambo ambalo kila mtu analipenda, huyo anaweza akaja kubadili mawazo ukijifungua na kuja kumuona huyo mtoto.

    Sasa hivi ww jitulize, na usiwe na papara naye, akikuandikia mjibu kwa kawaida tu, usitumbukize neno la marejeo.
    Chamuhimu, uwe karibu na Mungu wako!

    JibuFuta
  5. kwanza pole sana dada ila achana na huyu asema alikuwa na lake jambo, wewe lea mimba hadi mtoto wanaume ndio walivyo umeshafanya kosa hapo jitahidi sana usirudie kosa la pili.

    Always a child is gift and all mothers a gifted to have children no matter what hard ship they go through always your child will get the first priority, what you need to do is close your eyes and move on don't look back even if you love the guy and if you push it you will get hurt even more,

    pole sana

    JibuFuta

Unakaribishwa kutoa maoni yako.