Pages

Jumatano, Septemba 26, 2012

UJUMBE WANGU WA LEO UNAPOKUWA NA HASIRA NI VYEMA KUTULIA KABLA YA KUCHUKUA HATUA YOYOTE

Hasira ni sehemu ya maisha ya binadamu maranyingi mimi ninapokuwa na hasira huwa sipendi kutoa maamuzi huwa natulia na kutafakari kwanza, ijapokuwa inaweza kuwa ni vigumu inategemea na jambo ambalo limesababisha wewe kuwa na hasira kama kuna mtu amekukera amekusema vibaya au mpenzi wako amekukera basi ni vyema kutulia kabla ya kuchukua maamuzi kwani unaweza kujikuta unafanya jambo ambalo litakuumiza zaidi hapo baadaye. UNAAMBIWA TAFAKARI KABLA YA KUTENDA HASIRA NI HASARA

duuuuuh hasira hasara unaweza kuamua kupigana ukapigwa wewe lol

Maoni 2 :

  1. Kweli unayosema! Busara na uvumilivu wa moyo ni jambo zuri sana katika maisha ya binadamu.
    Hasira inaweza kuja kama radi inavyopiga! Lakini jiulize kwanza kabla ya kufanya kitu kilicho kuuzi.
    Nikipigana hapa sasa hivi au nikiacha ntapungukiwa na kitu gani? Mkalishe chini aliekukosea na umwambie, tafazali sana naomba tuongee wote kwa upole bila hasira tumalize tatizo hili mimi ni binadamu na wewe ni binadamu! Hakuna binadamu aliyekamilika! Naomba sana ulitambue jambo hili tuweze kumaliza hili tatizo! Labda we ulifanya uamuzi sio sahihi au mimi nilifanya hivyo pia.
    Jishushe chini na utumie hekima na busara nafikiri mwenzako nae atalitambua neno lako na suluhu itapatikana.

    JibuFuta
  2. Mpendwa tupo pamoja, nakuona hapo juu, unawaza kiutu uzima, maana hii picha imetoka `kiutu uzima'

    JibuFuta

Unakaribishwa kutoa maoni yako.