Pages

Alhamisi, Novemba 22, 2012

PENDELEA KUNYWA MAJI MENGI ZAIDI KULIKO KILEVI AU SODA AMA JUICE

Wataalamu wanakuambia ni vyema kunywa maji kila siku walau lita nne kwa siku lakini kwa kiasi kikubwa mtu huweza kunywa soda nyingi amba kilevi cha aina fulani kwa kiasi kikubwa kuliko kunywa maji. lakini maji  ni mazuri zaidi kiafya  na pia inashauriwa unapoamka asubuhi kabla ya kusafisha kinywa kunywa  glasi nne za maji yasiwe ya baridi ni mazuri sana kwa afya na pia husaidia kulainisha choo kwa wale wenye matatizo ya tumbo .

yafanye maji kuwa kilevi chako kwani husaidia pia kunyevusha ngozi na kuifanya ngozi yako kuwa laini na ya kuvutia .  Kuna watu inaweza kuisha siku nzima bila kunywa maji hata kidogo kwa kufanya hivyo unahatarisha usalama wa afya yako kwani maji yanasaidia vitu vingi mojawapo ni kusafisha mkojo na kuepukana na magonjwa kama U.T.I

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Unakaribishwa kutoa maoni yako.